CHIKAWE ATOWA MSAADA WA MABATI 100.

         Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia),    akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Nditi, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za  CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo ya Nditi wakati alipofanya ziara  katika kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya  Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. 


     Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia),      akimkabidhi jezi za timu sita za mpira wa miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu kwa ajili ya  kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika Kata hiyo katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa    mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo  jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikiangalia kifusi cha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni akifanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea mkoani Lindi. ( Picha zote na Felix Mwagara)

Post a Comment

Previous Post Next Post