IJUE HOME TEAM FOOTBALL ACADEMY; KITUO KIPYA CHA UKUZAJI VIPAJI KWA VIJANA KATIKA MPIRA WA MIGUU.

        Team ya Home Team Football Academy wakiwa katika picha ya pamoja kwenye                                                          Academy yao iliyopo maeneo ya Tabata.
                                           
                                             PICHA NA Mr. Verbs wa habarika24 blog
               Team ya Home Team Football Academy wakiwa uwanjani katika mazoezi
                Mazoezi ya team ya Home Team Football Academy wakiendelea na mazoezi
Home Team Football Academy ni akademi iliyoanzishwa kwa ajili ya kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa vijana na watoto wa rika mbali mbali kuanzia umri wa miaka mitano ‘5’ hadi kumi na saba ‘17’ na umri wa miaka 18 hadi 21.

 Pia kujenga timu itakayo shiriki mashindano mbali mbali ndani na nje ya Tanzania pamoja na kutoa wachezaji mahiri katika tasnia ya mpira wa miguu nchini. 

Licha ya kuwa timu ya mpira wa miguu pia inajumkumu la kujenga mahusiano bora katika jamii pamoja na afya ya vijana kupitia mazoezi na michezo.

Timu hii imeanzishwa mwaka 2009 hadi 2010 ilipovunjika na kisha baadae mnamo Octoba 2015 ilipoanzishwa upya chini ya waanzilishi wawili; kocha mkuu wa timu Said Ally na Raisi wa timu Sadiki Mshana kwa lengo la kukuza vipaji vya mpira wa miguu vya watoto na rika la makamu kwa kuzingatia sheria na katiba ya (TFF-Tanzania Football Federation) shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ya vijana chini ya umri uliotajwa hapo juu pamoja na kanuni za Shirikisho la mpira wa miguu wilaya ya Ilala, Dar es Salaam (IDFA-Ilala District Football Association).

JINA:                                      HOME TEAM FOOTBALL ACADEMY
MAKAO MAKUU:              TABATA KIMANGA
SIMU:                                    +255(0) 658 032 838/717 536 318
ANUANI PEPE:                   hometeamfootballacademy@gmail.com

RAIS WA TIMU: SADIKI MSHANA                           
  KOCHA MKUU: SAID ALLY


1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post