TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Msumbiji `Black Mambas` katika mchezo wa kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON, mwakani nchini Morocco.
Msumbiji walipata penati katika dakika ya 47 iliyozamishwa nyavuni na mshambuliaji tegemeo, Elias Gasper Pelembe.
Dakika ya 65 Khamis Mcha `Vialli` aliyetokea benchi na kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa, aliunganisha krosi iliyochongwa na Shomary Kapombe na kuisawazishia Stars bao hilo.
Dakika 6 baadaye, Stars ilipata penati na Mcha akafungga bao la pili na la kuongoza.
Dakika za lala salama, Stars walifanya shambulizi kali ambapo mpira uliopigwa na Thomas Ulimwengu uligonga mwamba, lakini Msumbiji walitumia muda huo kufanya shambulizi la kushitukiza na kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho.
Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Taifa stars kujisahau na Mambas wakatumia muda huo kuwaadhibu.
Kwa matokeo hayo, Stars inahitaji ushindi wa aina yoyote ugenini au kutoka sare ya mabao 3-3 ili kufuzu hatua ya makundi.
Post a Comment