KAULI YA HAKI ZA BINADAMU(LHRC) JUU YA UONGOZI WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA.


Mkurugenzi mkuu wa LHRC Bi. Kijo Bisimba Akiongea na waandishi wahabari.

Na Mwandishi wetu.
Kituo cha sheria na haki za binadam kimewatupia zigo la lawama kwa uongozi wa bunge maalum la katiba linaloongozwa na Mh Samwel Sitta kwa kitendo chao cha kushindwa kusimamia misningi ya uongozi bora hadi kufikia hatua ya utengenezaji wa katiba mpya ya Tanzania kuingia katika Mkwamo mkubwa ambao kwa sasa unaendelea kushika kasi
Akizungumza katika mkutano na waandish wa habari hivi leo tarehe 7.08. 2014.

 Mmoja wa wanaharakati na mpigania haki maarufu wa taifa hili B.Anenelia Nkya amesema  mkwamo ambao kwa sasa unaonekana dhahili kuhusu kupata katiba mpya umesababishwa bna uongozi mbovu wa Mh.Samweli Sitta na kuongeza kuwa rais Wa Tanzania anaonewa  pasipo sababu yoyote.

Nkya anafafanua zaidi kuhusiana na kutupa lawama hizo kwa Samwel Sitta Kuwa kiongozi huyo mkuu wa Bunge maalum la Katiba ndiyo msemaji mkuu katika bunge hilo sasa iweje yeey anakuwa legelege na kuruhusu mambo ambayo mpaka sasa taifa linapoteza mabilioni ya shilingi huku tukijua wazi kuwa kupata katiba mpya ni Ndoto ya mchana kweupe.

Nkya anaendelea anasema, Muhimili muhimu kama bunge hilo halikupaswa kuteteleka katika kusimamia haki na kanuni za bunge hilo , lakini Sitta ameshindwa kuzisimamia na ndio maana mpaka sasa tayari Mchakato huo umeingia njia panda.

Tokea Samwel Sitta kuruhusu Mh Rais awe wa mwisho na walioba awe wa kwanza ndio chimbuko la mkwamo ulipoanza na hapo ndipo Samweli Sitta alipoanza kuonyesha udhaifu wake wa kiuongozi, kwani angekataa mabadiliko hayo taifa lisingekuwa katika mkwamo wa kupata katiba mpya,

Mbona mwenzake Joseph Sinde Walioba aliweza kusimamia misingi ya uongozi bora na tume ilifanikiwa kuwa huru kwa kiasi kikubwa weje leo, Sitta anashindwa kusimamia taasisi hiyo muhimu ya kutengenrza katiba iwe huru ili tupate katiba alihoji Bi. Nnkya.
"Samweli Sitta hafai hata kuongoza nyumba kumi, iweje yeye akiwa kama mkuu wa bunge maalum la katiba anayumbishwa na watu ambao hawana mamlka na kama alilazimishwa si angesema na kujiudhuru nafasi hiyo tujue kuwa jamaa alilazimishwa sasa anakuwa kama mtu ambaye anatumika tuu huyu si kiongozi wa kutuongoza" Aliongeza B. Nkya

Naye kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadam, Bi. Kijo Bisimba ametoa wito kwa Bunge maalum la katiba kuheshimu uhuru wa kutoa maoni na kupokea habari  kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ili watanzania wapate fulsa ya kujadili mwenenndo wa uundaji wa katiba hapa nchini
Hatua hiyo imekuja kufuatia mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchmbi kutangaza hadharani kupiga marufuku mikutano yoyote yenye lengo la kujadili mchakato wa katiba nje ya Bunge maalum la katiba.

Hatua hiyo imetajwa kama ni hatua iliyolenga kuwaziba midomo wananchi wasijadili mwenendo wa mchakato wa katiba na kusema hatua hiyo ni kinyume na katiba mama ya jamuhuri ya muungano wa TANZNAIA ya mwaka 1977.

Post a Comment

Previous Post Next Post