Diamond Platnumz akipokea tuzo.
Diamondi ndiye msanii aliyeweza kuiwakilisha na kuitanagaza vema nchi yetu ya Tanzania katika sekta nzima ya
tasnia ya mziki hasa hasa mziki wa kizazi kipya alimaarufu kama Bongof leva.
Siwezi kumsahau dada yangu Lady Jaydee, ambaye ni mwanamuziki mkongwe
na mwenye heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania katika tasnia hii ya mziki.
Jaydee ndiye msanii pekee mkongwe aliyeweza kusimama imara na kushika
nafasi ya juu kwasasa katika tasnia ya mziki kuliko wasanii wote nchini, na
ndiomaana bado anapata tuzo zenye hadhi ya juu Africa. Ingawa najua wapo
wasanii wengi wakongwe wanaendelea kufanya vizuri mpaka sasa, kama vile akina
AY, Profesa J, Mwana FA n.k, ila kwa muda huu bado dada yangu Lady Jaydee ndiye
anaye wakimbiza wakongwe wote kwasasa.
Haijalishi ni kwa Wanaume au Wanawake ila ni Lady Jaydee tu ndiye
msanii mkongwe anaeendelea kuipeperusha vema bendera na kuitangaza nchi yetu ya
Tanzania katika fani ya mziki, kwa uthibitisho ni juzi kati tu yeye na Diamond
wameleta tuzo za heshima nchini.
Ndugu zangu, naomba ifahamike kwamba, Diamond anae wika leo si msanii
mkongwe la hasha, bali ni msanii chipukizi aliyekuja kuwa Star.
Diamond ni Star na si Mkongwe
katika tasnia ya mziki, ila Lady Jeydee ni msanii Mkongwe na Star katika tasnia
ya muziki.
Naomba ifahamike kwamba ninapo zungumzia Star na Mkongwe, namaanisha
kwamba hawa ni watu wawili tofauti. Nikiwa na maana kuwa; kuna utofauti wa Star
na Mkongwe, mfano; Msanii mkongwe ni mtu
aliye kaa kwa muda mrefu katika fani hiyo, mtu kama vile; Afande Sele, Hadija Kopa, Juma Nature, Lady Jaydee, Profesa J, n.k, hao ndio wakongwe. Ila unapomzungumzia mtu
kama Diamond, Ommy Dimpoz, Ally Kiba, Barnaba, n.k, hawa ni wanamziki
waliochipukia ila ni Masatar. Nadhani nimeeleweka, utofauti wa Star na Mkongwe
japo kwa ufupi.
Katika Makala yangu hii ya Nyota wa wiki mimi nimemchagua Diamond, msanii chipukizi lakini STAR mkali, huyu ndiye
nyota wa wiki katika blog yenu muipendayo ya HABARIKA24.
Diamond anakila sababu ya kuwa Nyota (Star) kwa mtazamo wangu, kwani
mpakasasa ndiye msanii pekee aliyeweza kuitambulisha na kushiriki tuzo kubwa za
mziki kuliko wasanii wote nchini wote Tanzania.
Diamond Pia ndiye msanii anaye tambulika zaidi Kimataifa kuliko msanii
yeyote nchin.
Diamond huyo huyo ndiye msanii aliyeweza kuibuka mshindi wa tuzo zenye
heshima kubwa barani Africa zinazo julikana kama African Music Magazine Awards,
ambazo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko
Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo
Diamond mwenyewe wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo hizo.
Diamond
ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni
wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one remix’ alioufanya na Davido wa
Nigeria.
Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
So why not
Diamond to be HABARIKA24s’ STAR?
Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Kwa mujibu wa africanmuzikmag.com Producer bora wa mwaka alishinda Dj Oskido wa South Africa aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda, Sheddy Clever wa Tanzania na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video ilichukuliwa na Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Salamu na ushauri kutoka habarik24.blogspot.com
Usibweteke kwani huu ndio mwanzo, tayari dunia
imekutambua na imetambua uwepo wa Watanzania katika ushinda wa soko la mziki
kidunia. Hivyo wenzio tayari wameanza kujipanga kwa ajili yako kwenye
kinyanyiro cha mwakani. Hivyo anza kujipanga na wewe. Usipoteze muda kwenye
usama wa kipropaganda bali poteza muda kwenye uhsama wa kugombea na fasi ya
kuwa Mfalme wa kiduni katika fani yako. Ni hayo tu.
Mungu
ibariki Tanzania,
Mungu
tubariki Watanzania,
Mungu
ibariki afrika kwa ujumla,
Asanteni
sana.
Post a Comment