Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Taasisi ya kifedha ya UTT Microfinance, baada ya kukata utepe kuzindua taasisi hiyo, Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya huduma za Kifedha ya UTT Microfinance, Dar es Salaam jana. Wa pili Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Balozi Fadhili Mbaga na Mtendaji Mkuu wa UTT, Bw. James Washima (kushoto).
Naibu Waziri wa Fedha Bw. Mwigulu Nchemba (katikati), akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kifedha ya UTT Microfinance, Bw. James Washima wakati akimuonyesha vipeperushi, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Fadhil Mbaga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kifedha ya UTT Balozi Fadhil Mbaga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima wakimwangalia Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba.
Naibu
Waziri Fedha aifagilia UTT Microfinance
NAIBU
Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imevutiwa na
utendaji kazi mzuri wa Taaisisi ya kifedha ya UTT Microfinance kuwa na matawi
10 katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa muda mfupi.
Akizungumza
wakati wa kukata utepe kuzindua rasmi Taasisi hiyo Sukari House Dar es Salaam
jana, Naibu Waziri amesema, Serikali imefurahishwa na dhamira ya kweli ya
kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi kila pembe ya nchi kunakofanywa
na UTT.
“Hii
inaonyesha, mmeshaanza kutoa aina nane ya huduma kama mikopo, uwakala wa Bima,
Uwakala wa Benki, uwakala mkuu wa mitandao ya simu (mobile money super
agent) kwa mwaka mmoja tangu kuanzishwa”.
Bw.
Nchemba amesema, kazi kubwa iliyoifanya ndani ya muda mfupi na kuwa na matawi
10 katika maeneo mbalimbali ya nchi yameifurahisha na kuahidi kuwa Serikali
itatoa ushirikiano wa karibu kwa taasisi hiyo ili iweze kufikia malengo
iliyokusudia.
Naibu
Waziri amebainisha kuwa uwa serikali iliamua kwa makusudi kuanzisha taasisi
hiyo ili kuwezesha wananchi kiuchumii hususan wenye miradi, kama biashara
ndogondogo na za kati ambao wamekuwa wakipata changamoto nyingi katika kupata
mikopo na huduma nyingine za kifedha toka taasisi kubwa za kifedha na
mabenki ya biashara ambayo mara nyingi muundo na mfumo wa taasisi hizo
huambatana na masharti magumu.
“Wengi
walishindwa kupata mikopo stahiki kutokana na masharti, hususani wenye vipato
vya chini, sharti la dhamana ya mali isiyo hamishika kama nyumba, kiwanja na
mali, ambavyo hawana”, anasema Bw. Nchemba na kusisitiza kuwa Serikali
imeanzisha UTT Microfinance kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwainua watanzania
walio wengi.
Awali
kabla ya uzinduzi huo, UTT Microfinance imezindua rasmi mtandao wa matawi
sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kufikisha huduma za kifedha karibu na
wananchi hususan mikopo nafuu kwa wajasiriamaliri ambapo matawi 10 yaliyopo
katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar
ulizinduliwa rasmi katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali, wakurugenzi wa mashirika, Makampuni na Taasisi mbalimbali pamoja na
wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa
upande wake, Mweneykiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT MFI Balozi Fadhili Mbaga,
alisema watahakikisha kuwa UTT MFI inatekeleza azma yake kwa ufanisi na pia
itashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali.
“Tunapenda
kusisitiza dhamira yetu ya kuendelea kushirikaiana na wadau mbalimbali hususan
Tanzania Microfinance Association katika jitihada za jumla za kuwa na mfumo
mzuri wa huduma za kifedha na mitaji midogo na kuhakikisha kuwa huduma hizi
zinawafikia watanzania wengi zaidi na kuwa chachu muhimu ya maendeleo ya jamii
yetu”, anasema Balozi Mbaga.
Ameishukuru
serikali kwa ushirikiano inayotoa kwa taasisi hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi
changamoto zilizo mbele yao kuhakikisha wanavuka malengo waliyojiwekea.
ameiomba serekali isisite kuwaunganisha na wabia na washirika mbalimbali ili
kuwa na mtandao mpana zaidi wenye nguvu ya kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa UTT MFI James Washima, alisema wanaamini Serikali
haikufanya makosa hata kidogo katika kuanzisha UTT MFI, akiahidi kututumia
uzoefu wao wa mwaka mmoja, ambao umebaini kuwa huduma za kifedha na mikopo
hususan kwa wajasiriamali na watanzania wa kada za kati na chini zilisubiriwa
kwa hamu kubwa sana.
Bw.
Washima amesema kiu ya Watanzania kwa huduma za UTT hivyo taasisi yao
imejipanga kutoa huduma nzuri. Ameahidi kuwa ndani ya miezi sita wataongeza
idadi ya wafanyakazi kwani waliopo ni wachache ambapo mfanyakazi mmoja
anahudumia wateja zaini ya 1,000.
“Huu
ni muitikio mzuri kutoka kwa jamii na sisi tunajitahidi kukabiliana nao kwa
ufanisi” anabainisha Bw. Washima na kuongeza kuwa hivi sasa wana matawi
10, manne yakiwa Dare s Salaam - Sukari House, Azikiwe, Kijitonyama na
Chang’ombe.
Bw.
Washima anayataja matawi mengine kuwa ni Arusha lililopo Ngarenaro, Meru
lililopo Jengo la Posta Meru, Dodoma lililopo Posta Dodoma, Mbeya
barabara ya KKKT, Mwanza katika jengo la Posta na Zanzibar, Jengo la Posta
Kijangwani.
Akizungumzia
m,afanikio ndani ya mwaka mmoja wa uwepo wao, Bw. Washima anasema wameweza
kukuza mtaji wa Taasisi toka Shilingi billion 5.4 mnamo Julai mwaka 2013
na kufikia bilioni 12 Juni, 2014. Pia taasisi imefanikiwa kutoa mikopo
yenye thamani ya Tsh 5.316 bilioni,
kwa wakopaji 6,102 – huku 84% ya wakopaji wote wakiwa ni wanawake.
Anabainisha
kuwa pia wameanzisha huduma za moja kwa moja kwa muhusika (Tailor-made) kama
vile mikopo kwa ajili ya Bima ya matibabu, Hati Malipo (Contract Financing
loans), mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo (Group loans),
Mikopo kwa ajili ya SACCOS, Mikopo maalumu kwa miradi inayolenga kuongeza
thamani ya bidhaa na ajira ikiwemo viwanda vidogo vidogo, mikopo kwa
wafanyakazi wa Serikali.
Hata
hivyo, pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, Washima alieleza baadhi ya
changamoto zinazowakabili ikiwa kuibuka kwa taasisi na kampuni zisizo rasmi
ambazo hutoa huduma za kifedha hususan mikopo kwa watu wa kada za chini.
Mtendaji
huyo amesema mengi ya makampuni haya mara huwa ya kilaghai na yenye kuchukua
riba kubwa bila utaratibu maalum suala ambalo badala ya kuwasaidia watu,
huwaumiza na kuwaua kabisa kiuchumi.
“Tunaiomba
serikali iharakishe utungwaji wa sera ya kurasimisha huduma hizi ili zifanywe
kwa utaratibu maalum na pia ziratibiwe na kudhibitiwa vizuri ili wananchi
wasiendelee kutaabika na kufilisiwa na watu wasio na nia njema ambao hutumia
fursa ya udhaifu wa kisera kujinufaisha” alisema Washima.
UTT MFI
ni Taasisi ya huduma za fedha na mikopo iliyoanzishwa mnamo Juni 2013 kwa lengo
la kutekeleza sera za serikali katika uwezeshaji kiuchumi hususan kwa
wajarisiamali, watumishi wa umma, wakulima, wenye viwanda vidogo, watu wasio na
ajira rasmi na wananchi wote kwa ujumla.
UTT MFI
pia inalenga kuwapa fursa wamiliki wa Vipande vya UTT AMIS kutumia vipande vyao
kama dhamana wakati wa kuchukua mikopo, kupanua wigo na kurahisisha uwekezaji
wa vipande vya UTT na hivyo kukuza utamaduni wa kuwekeza kwa wananchi.
Post a Comment