Kipimo Abdallah
Alitoa wito kwa watanzania kuviunga mkono vyama vya siasa ambavyo vinaonyesha ni madhubuti ya kukabiliana na ubadhirifu wa rasilimali za Taifa ili kufikia malengo ya maisha bora ambayo kwa sasa yamekwama.
Katibu huyo wa Mawasiliano na Uenezi alisema iwapo vyama vya upinzani vitakuwa na umoja na ushirikiano wa dhati zipo dadli tosha za kukiondoa chama tawala madarakani.
CHAMA
cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimekanusha
tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa ni chama kilichokuja
kubomoa vyama vya upinzani hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu wa
Mawasiliano na Unezi wa ACT -Tanzania Mohammed Massaga wakati
akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana ofisi kwake jijini Dar es
Salaam.
Massaga aliomba vyama hivyo
kuacha kufanya siasa nyepesi na kujikita katika hoja ili kuhakikisha
kuwa upinzani unakuwa na nguvu ili viweze kukitoa chama tawala CCM
madarakani.
Alitoa wito kwa watanzania kuviunga mkono vyama vya siasa ambavyo vinaonyesha ni madhubuti ya kukabiliana na ubadhirifu wa rasilimali za Taifa ili kufikia malengo ya maisha bora ambayo kwa sasa yamekwama.
Katibu huyo wa Mawasiliano na Uenezi alisema iwapo vyama vya upinzani vitakuwa na umoja na ushirikiano wa dhati zipo dadli tosha za kukiondoa chama tawala madarakani.
Alisema wapo baadhi ya viongozi ambao wanashindwa kufanya siasa na kubakia kulalamika jambo ambalo linachelewesha mabadiliko.
“Ndhani unaona mwenyewe tatizo la
siasa za Tanzania ni wanasiasa kushutumiwa na kuacha kufanya siasa za
kweli ambazo zinaweza kuleta mabadiliko kwa jamii ya Kitanzania” alisema
Massaga alitolea mfano wa
mchakato wa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kuwa ni
matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Kwa upande mwingine Massaga
alisema katika kujenga chama chao cha ACT- Tanzania wamefanikiwa kuvuna
wachama wapya zaidi ya 11,800 katika mikoa 12 ya Tanzania Bara kwa
kipindi cha mwezi Agosti mwaka huu.
Katibu huyo wa Mawasiliano na
Uenezi ACT alisema kwa sasa chama hicho kina wanachama zaidi ya 187,000
nchini kote hivyo juhudi zao ni kuongeza wanachama wengi zaidi kwa
kutumia itikadi yao ya demokrasia ya jamii.
Alisema chama hicho kilifanya
ziara katika mikoa 12 ambayo Tanga, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita,
Tabora, Mara, Mwanza, Lindi, Kigoma, Pwani na Mtwara ambapo wamepokelewa
kwa nguvu kubwa.
Massaga alisema pamoja na kuvuna
idadi hiyo ya wanachama wamefanikiwa kusimika viongozi wa muda katika
majimbo 68 ya Tanzania bara na viongozi wa kata na matawi kwenye majimbo
hayo.
“Kwa kifupi tumepata mafanikio
makubwa katika kipindi hiki cha miezi minne tangu kupewa usajili wa muda
kwani kila tunapopita tunapokelewa kwa nguvu zote jambo ambalo linatupa
matumaini ya kufanya vizuri kwenye chaguzi zijazo”, alisema.
Katibu huyo wa Mawasiliano na
Unezi wa ACT-Tanzania alisema katika kuhakikisha kuwa wanafikia malengo
katika medani za siasa Tanzania wataendelea kuwaelimisha wanachama juu
ya kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Post a Comment