AZANIA BENKI WAZINDUA AKAUNTI MPYA YA DHAMIRA (MSIKILIZE MKURUGENZI-VIDEO).


MKURUGENZI mtendaji wa Azania benki,Charles Singili amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadae.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira, Singili amesema kuwa utaratibu wa kujiwekea akiba utapunguza tatizo la umasikini kwa wananchi.
 
Aliongezea kuwa, endapo wananchi wakipatiwa elimu kuhisu faida za kutunza fedha zao,itasaidia kupunguza hali ya umasikini uliopo sasa.
 
“Kwa kutambua matatizo yanayoikabili nchi yetu, Azania bank imeamua kufungua akaunti ambayo itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote” alisema Singili.
 
Singili aliongezea kuwa, akaunti ya Dhamira, itamsaidia mwananchi yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwenzi.
 
Aliongezea kuwa, akaunti hiyo inatafunguliwa na mtu ambae ametimiza miaka 18 na kuendelea na itamsaidia kuweka riba kadri awezavyo.
 
“Dhamira akaunti itamsaidia mwananchi kutimiza malengo au ndoto zao, pia kipindi cha chini kuweka akiba ni miezi 12,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira (Dhamira Account) uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo,Ubungo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wakimsikilizwa kwa makini Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Azania.

Post a Comment

Previous Post Next Post