Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa wanafanya mahojiano na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia leo jijini Arusha katika studio za redio 5
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Kusini ,akiongea na waandishi wa habari leo jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu njiro ambapo alisema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015.
Habari picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya ubunge
Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa bado hajawa na ndoto ya kuwa Rais 2015
Alisema kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu
”Pamoja na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu sana”alisema Nkamia
Pia Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo.
Mkurugenzi wa Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis akiwa anamsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia wakati akizungumza na waandishi wa habari kulia ni mwandishi wa chanel Ten Jamilah Omary
Mtangazaji wa redio 5 Mwangaza Jumanne akifanya mahojiano live na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma NkamiaMeneja masoko wa Tan Communication media Bi.Sarah Keiya akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia.

Waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa kituo cha redio 5 Bw. Robert Francis katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia, kulia ni mmiliki wa mtandao wa Jamiiblog Pamela Mollel.
Post a Comment