Kibao / Nembo ya Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Nsimbo.
(Picha na Kibada kibada –Nsimbo Mlele).
Na Kibada Ernest Kibada Mpanda Katavi.
SEHEMU ya eneo la Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo , Mlele Mkoa wa Katavi limeuzwa kwa wakandarasi wanaotengeneza barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Sitalike hadi Mpanda Mjini .
Eneo hilo la shule limeuzwa kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Kichina lijulikanayo kwa Jina la Railway Sevanth Group lenye Makao yake jijini Dar es salaam.
Eneo hilo limenunuliwa kwa ajili ya kuchimba kifusi kinachotumika kutengenezea barabara ya lami inayoendelea kujengwa kutoka Kata ya Sitalike hadi Mpanda Mjini.
Akizungumzia kuhusu eneo hilo kuuzwa kwa Mkandarasi huyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Magamba Mwl. Yohana Kasansa ameeleza kuwa yeye hatambui kuuzwa kwa eneo hilo bali anatakumbua kuwani eneo halali la Shule.
Akaeleza kuwa yeye anaona tu shughuli zikiendelea za uchimbaji wa kifusi kwa ajili ya kutengeneza barabara lakini hajui nani alitoa ruhusa.
Alisema eneo hilo la shule hutumika kwa ajili ya kulima mazao aina ya mahindi kwa ajili chakula cha shule kwa watoto.
Mwalimu Kasansa akaongeza kuwa wakati linapokuwa halitumiki kwa ajili ya kilimo huwa linaachwa wazi lakini baada ya kuchimbwa udongo kwa ajili ya kifusi limebaki na mashimo ambayo ni hatari kwa watoto na hasa wakati huu ambao mvua zinapokaribia kunyesha.
Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Magamba George Pius alipotakiwa kuelezea uuzwaji wa eneo la Shule ambayo ni mali ya Kijiji, alisema kuwa hatambui ni nani aliuuza.
“Kufuatia hali hiyo niliwaandikia barua ya kuwataka wasitishe shughuli za kuchimba kifusi katika eneo hilo ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lakini hawakutekeleza na waliendelea na kazi kama unavyoona hapo kazi zikiendelea”alisema Pius Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Magamba.
Eneo la Shule ya Msingi Magamba ambalo linadaiwa kuuzwa kwa wakandarasi wanaotengeneza barabara ya Sitalike –Mpanda kwa Kiwango cha lami likichimbwa kifusi.
Post a Comment