Katibu na Mwanasheria mkuu wa kampuni ya ufuaji umeme ya IPTL, Bw. Joseph Makandege akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) nakala ya hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania ikizuia benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Tanesco kuendelea kuwabugudhi wamiliki wa IPTL na kuingilia uendeshaji wa mitambo yake. Kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa IPTL Bw. Aidan Kaude.
· Yasema
Bw. Sethi kuendelea kusimamia mitambo ya ufuaji umeme ya Tegeta.
Mahakama Kuu ya Tanzania imeiamuru Benki ya
Standard Chartered ya Hong Kong na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania
(TANESCO) kuacha kuingilia utulivu, umiliki,
usimamizi na utawala wa Mitambo ya ufuaji umeme ya Bw. Harbinder Singh Sethi
iliyopo Tegeta, na kusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya msingi.
Kampuni ya Independent Power
Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions Limited (PAP) zilifungua
kesi kwa kuhoji uhalali wa maamuzi ya Kituo cha Kimataifa cha Kutatua Migogoro
ya Uwekezaji (ICSID) dhidi ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK)
na Martha Renju (anaedaiwa kuwa msimamizi wa mali zake), ijulikanayo kama
"Decision on
Jurisdiction and liability" iliyotolewa katika kesi ya ICSD
namba ARB / 10/20.
Katika hukumu hiyo yenye
kurasa 16 iliyoandikwa na Mhe. Dk. Fauz Twaib (Jaji) na kusomwa kwa niaba
yake na Mhe. Amri Msumi Hamisi (Jaji), mahakama kuu jana iliwazuia SCBHK na /
au Tanesco kuendelea kuwabugudhi IPTL na PAP -zinazomilikiwa na Bw. Sethi –
mpaka pale uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya msingi itakapo amuliwa.
Katika hukumu hiyo
iliyotolewa na mahakama mbele ya Bw. Sethi (mmiliki wa IPTL / PAP)
na Kieren Day (Mkurugenzi wa SCB-HK), Mhe. Dk Twaib aliamuru Tanesco kutofanya
biashara yoyote na SCB-HK au Martha Renju kwa niaba ya IPTL / PAP bila ya
idhini ya kimaandishi kutoka IPTL / PAP.
"Wadaiwa kwa pamoja
wanazuiliwa kufanya utekelezaji wa maamuzi iliyotolewa katika chombo cha
kimataifa ya ICSD yenye namba ARB / 10/20 na kusambazwa kwa wahusika mnamo
tarehe 12 mwezi Februari mwaka 2014, kwa namna yoyote ile, na kusubiri
uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya mdai, " inasomeka sehemu ya hukumu hiyo.
Tanesco ambayo
iliwakilishwa na Wakili wake Bw. Urassa, pia imezuiwa kutolipa kwa SCB-HK na
Martha Renju malipo yoyote wanayostahili IPTL / PAP bila ya idhini ya maandishi
kutoka kwa IPTL / PAP.
Mahakama pia imeizuia Tanesco kutotekeleza
au kukubaliana
na au kuyatekeleza maamuzi ya ICSID, na kusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yao
ya msingi.
Jaji Mhe. Dk Twaib
alitupilia mbali hoja ya mwanasheria wa SCB-HK, Bw.Charles Morrison, ambaye
alisema kuwa mahakama kuu ya Tanzania haipaswi kusikiliza na kutoa maamuzi juu
ya ombi hilo sababu Tanzania ni mwanachama wa Kituo cha Kimataifa cha Kutatua
Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) ambayo pia inajulikana kama Washington Convention au ICSID .
Kwa mujibu wa hakimu Dr.
Twaib, Wakili Morrison alionya kuwa kama Tanzania aitotii wajibu huo,
itajiweka sehemu mbaya katika nyanja ya kimataifa.
"Kwa heshima
kubwa, nashindwa kuona mantiki ya utetezi wa Bw. Morrison na jinsi gani
litaathiri mamlaka ya Mahakama hii la kuikubali ombi hili. Japokuwa Bw. Morrison
amekwepa kusema moja kwa moja, maoni yake yamelenga kusema kwamba mahakama hii
haina mamlaka ya kutoa amri husika.
"Ninashindwa kuelewa
ni jinsi gani serikali ya Tanzania, ambayo si sehemu ya kesi hii, itakuwa
imevunja Mkataba wa Washington kwa sababu tu ya wananchi wake wawili ambao ni
wafanyabishara binafsi, wametafuta amri ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa
ICSID kwa misingi ya udanganyifu. Sioni ni jinsi gani, kwa kutumia mamlaka yake
katika kutoa maagizo hayo, mahakama hii itakuwa inaingilia majukumu ya
kimataifa ya Tanzania chini ya Mkataba wa Washington," inasomeka hukumu ya
Jaji Twaib.
Sababu ya pili ya Bw.
Morrison ya kuoma mahakama isikubali ombi hilo ilikuwa kwamba madai hayo
yanaweza kuwa yametolewa “miaka mingi iliyopita” wakati kesi ya ICSID ilipoanza
na kubainisha kuwa hii ni kesi iliyokufa (tort case), ingekuwa imefanyiwa kazi
ndani ya miaka mitatu ya tarehe ile.
Jaji Twaib
alitupilia mbali hoja hiyo kwa kusema, "Kwa heshima kuba kwa Bw. Morrison,
hoja hii haina nguvu ya kisheria. Kama ilivyosemwa na mwanasheria wa waombaji
(Bw. Joseph Makandege na Bw. Melkzedek Lutema), madai hayo yanatoa changamoto
kwa uamuzi wa ICSID ambayo ulitolewa mwezi Februari, 2014. Madai, hayo baada ya
kushindwa Aprili 2014, haiwezi ukasema imepitwa na wakati. Nitaitupilia mbali
pingamizi hilo.”
Kuhusu ombi kuwa shauri
hilo lisikilizwe katika mahakama ya Hong Kong na fedha zote zipelekwe hiko,
wanasheria wote Bw. Makandege na Bw. Lutema walisema kuwa litakuwa sio
kutenda haki kwa mteja wao, sababu kuna kiasi kikubwa cha fedha kinahusika,
ambayo itakuwa vigumu kuirejesha na kuwa itakuwa vigumu kwa IPTL/PAP kurejea
katika hali yake kwa sababu SCB-HK ni ya nje na haina mali zozote kubwa
Tanzania.
Hii inampa Bw. Sethi
ushindi kwa mara nyingine miongoni mwa kesi kadhaa ambazo zimekuwa zikianzishwa
na SCB-HK dhidi ya IPTL/PAP.
·
Post a Comment