MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA YASSINI HEZRON (14) MKAZI WA KIWIRA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.235 AFB AINA YA M/CANTER LILILOKUWA
LIMEBEBA MATOFALI LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE FREDY MPONDO KUSHINDWA
KUPANDA MLIMA NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUANGUSHA MATOFALI NA KUSABABISHA
KIFO KWA TINGO HUYO.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
29.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MAENEO YA NEW LAND BAR, KATA
YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA TUKUYU/KYELA. CHANZO CHA AJALI NI GARI HILO KUSHINDWA
KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO
HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. OTHAZ ANGOLILE
(18) 2. SAMSON MWANGOMILE (46) 3. FORD SAMSON (20) NA 4. BARAKA JOSEPH
(23) WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS NA RIDDER PAKETI 108.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI
HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO NA TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA/KUUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment