BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE WA VITI MAALUM,VIJANA -MBEYA ,ATOA VIPAUMBELE VYAKE.

Bi. Chikulupi Njelu Kasaka 
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu
 Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto)  na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu

                  MFAHAMU BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA

*Anaitwa Chikulupi Njelu Kasaka.

*Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.


*Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT
.
*Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).


*WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA

ELIMU:
Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha Mtanila katika Wilaya ya Chunya.

 Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka 2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo baadaye niliapishwa kuwa wakili.

UZOEFU KATIKA UONGOZI:
Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi - DARUSO.

 Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.

 Pia alikuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010 alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.

 Pia mwaka 2014 alishiriki mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo haya.

UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya kumaliza elimu ya sekondari 2006. 
Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu. Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.

KAZI:
Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao International Migration Management Program (IMMP). 

Mwaka 2012 aliajiriwa na Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma. 

Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.

VIPAUMBELE:
Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti Maalum-Vijana. 

Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu, bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo: 

ELIMU, AJIRA, MICHEZO, UTALII na AFYA.
ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.



Post a Comment

Previous Post Next Post