MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF), WAKUTANA NA WAHARIRI, DAR ES SALAAM

 MKURUGENZI Mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa Wahariri kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015

Na K-VIS MEDIA
MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari Nchini, kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015, kwa nia ya kujitambulisha na kuelezea mikakati yake ya kiutendaji na majukumu iliyo nayo.

Akiwasilisha mada kwa Wahariri hao, Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza wa Mfuko huo, Masha Mshomba, amesema, Mfuko huo umeanzishwa ili kutekeleza sheria ya fidia kwa wafanyakazi (Sheria namba 20, ya mwaka 2008.

“Majukumu ya Mfuko huu ni kuwasaidia wafanyakazi wanaoathirika kuweza kurudi kazini au kushiriki katika shughuli nyingine zitakazowapa kipato.” Alisema Mshomba na kuongeza kuwa majukumu mengine ni pamoja na kutunza kumbukumbu za matukio ya ajali, magonjwa na vifo vinavyotokana na kazi, ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu kazi za mfuko na manufaa yake.

Alisema, Mfuko huo ni mpya na kwamba unahitaji ushirikiano wa dhati kutoka vyombo vya habari na ndio maana Mfuko umeona umuhimu wa kukutana na Wahariri wa vyombo vya habari kwani wao ndio kiungo kati ya Mfuko na Umma.

Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, amesema, Mfuko huo umekuja kurahisisha ushughulikiwaji wa malalamiko ya fidia kwa wafanyakazi moja kwa moja bila ya kuanza kupitia sehemu nyingine.

Alisema, SSRA kama mama wa Mifuko yote, inao wajibu wa kuisaidia WCF katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria na Wahariri wa vyombo vya Habari ni kiungo muhimu katika kuhakikisha umma wa Watanzania unajua shughuli na kazi za Mfuko huo.

Naye kwa upande wake, Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena alishukuru WCF kwa kuwaalika wahariri ili kuwaeleza vema shughuli na majukumu ya Mfuko huo kwani vyombo vya habari ndio wakala wa Umma na taasisi za kutoa huduma kama WCF.

Ninawapongeza WCF kwa kuwa majasiri wa kuwaalika wahariri na kukutana nao na kupokea maswali yao, kwani taasisi nyingine huogopa kufanya hivyo tena katika hatua ya awali kama yenu. Alisema Meena

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, akifungua warsha hiyo
 Mhariri Shemax Ngahamera akizungumza kwenye warsha hiyo
 Mhariri wa vipindi wa ITV/Radio One, Steven Chuwa, (kulia), na Mhariri Mtendaji wa EFM, Scolastica Mazula, wakipitia mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF
 Mhariri Mshiriki wa gazeti la Nipashe, Ramadhan Mbwaduke, akiuliza swali
 Mhariri gazeti la Serikali, Sunday News, Ichikaeli Maro, akizungumza wakati wa warsha hiyo
 Baadhi ya Wahariri wakinukuu yaliyokuwa yakielezwa kwenye warsha hiyo
 Mhariri Anold Victor, akiuliza swali

 Mhariri mkongwe, Mzee Yasin Sadick, akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warsha hiyo
 Baadhi ya Wahariri, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa juu ya kazi na huduma zitolewazo na WCF
Mhariri  wa kujitegemea Mzee Wence Mushi akiuliza swali

Post a Comment

Previous Post Next Post