GLOBAL PEACE FOUNDATION, TAWI LA TANZANIA KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Viongozi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana  
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katka kipindi hiki  kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
 Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (kushoto) na  Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda, wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
 Ofisa Utawala wa Shirika hilo, Hilda Ngaja (kushoto) na Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu (kulia), wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

 Na Dotto Mwaibale

GLOBAL  Peace  Foundation Tawi  la  Tanzania  (GPFTZ), kwa kushirikiana  na    Mshirika  wake, Baraza  la  Wadhamini  la  Taasisi  ya  Viongozi  wa  Dini  Tanzania (IRCPT),  wamezindua  kampeni  ya  kuhamasisha  Amani  nchini  Tanzania  katika  kipindi  hiki  kuelekea  uchaguzi  mkuu  ,  jina  la  kampeni  ni  “Amani  Kwanza”.  

Lengo  kuu  la    kampeni hiyo  ni  kuhamasisha  watanzania  wote  kushiriki    katika  Uchaguzi  Mkuu  kwa  Amani  ambao  unatarajia  kufanyika  siku  ya  25/08/2015.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi  alisema Walengwa  wakuu  wa  Kampeni  hiyo  ni  Wanawake  na  Vijana ambao  ni  wengi  zaidi  ukilinganisha  na  rika  na  makundi  mengine,  na  pia  Wanawake  wamekuwa  wakihathirika zaidi  endapo  inapotokea  machafuko  hali kadhalika  Vijana  wamekuwa  chanzo        cha  uchochezi  wa  machafuko  katika  nchi  mbalimbali  duniani.
·         
"kampeni  hii  haina  lengo  lolote  la  kuunga  mkono    ama  kupinga  Chama  chochote  cha  Kisiasa  au  mgombea  wake,  na  wala  haina  mahusiano  yoyote  ya  kisiasa na kauli kauli  mbiu  yake ni “KURA  YANGU  UZALENDO  WANGU,  AMANI  YA  NCHI  YANGU  NI  JUKUMU  LANGU” alisema Nghambi.

Nghambi alisema Kampeni hiyo  imeandaliwa  maalumu  kwa  malengo  ya kuwahamasisha  Wanawake  na  Vijana  kuwa  mabalozi  wazuri  wa    kulinda  na  kuitetea  Amani  ya  nchi  yetu  hasa  katika  kipindi  hiki  kuelekea  uchaguzi Kujiepusha  na  vitendo  mbalimbali    ambavyo  vinaweza  kuchochea  uharibifu  wa  Amani  nchini Kuhamasisha  
kila  mmoja  ashiriki  uchaguzi  kwa  amani Ili  kuhakikisha.  

Alisema kampeni hiyo inafanikiwa  kutokana na Shirika  la Global  Peace kushirikiana kwa  karibu  na  vyombo  vya  habari  nchini  vikiwemo  Radio,  Luninga,  Magazeti,  na  mitandao  mbalimbali    ya  Kijamii  ikiwemo Twitter,  Face  Book,  instagram  na  YouTube.  


Alisema  shirika hilo ni Tawi  la  Taasisi  ya  Kimataifa  isiyo ya  Kiserikali  na  isiyotengeneza  faida  Global  Peace  Foundation  (GPF)  yenye  makao  makuu  yake    Washington  DC,  nchini  Marekani.    

Alisema  shirika  hilo linahamasisha  kutetea  na  kulinda  Amani  dunia  ,    shirika  hili  linaamini  ya  kuwa “ Kwa  Mungu  sisi  wote  ni  familia  moja” GPF  inafanya  kazi  kwa  karibu  na  mitandao  ya  kiserikali  na  watu  binafsi  katika  kuendeleza  jamii,  taifa  na  katika  kujenga  na  kulinda  misingi  na  maadili  katika  jamii  husika.

GPF  ina  rekodi  nzuri  ya  kufanya  kazi  kwa  karibu  na  kwa  mafanikio  makubwa    kuhamasisha  na  kulinda  Amani  katika  nchi  mbalimbali  dunia  katika  bara  la  Afrika,  Asia,  Ulaya  na  Amerika.

Kwa  upande  wa  Afrika,  shirika  hili  limekuwa  likijihusisha  na  maswala  mbalimbali  ya  kijamii  katika  nchi  za  Kenya,  Uganda  na  Nigeria  kudumisha  Amani  kwenye  ukanda  wa  Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post