HOTUBA YA MGOMBEA URAIS WA ACT-WAZALENDO MAMA ANNA MGWIRA YA WATETEMESHA UKAWA NA CCM.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam.
............................................................................................................
NA Mwandishi wetu- Mbagala DSM.
Mshehereshaji: ACT kinakuja kuleta mfumo mpya wa Vyama, ukihitaji siasa za Ulaghai, mbwembwe nenda chama Kingine.Ukitaka chama cha mikakati,chama cha siasa safi njoo ACT Wazalendo.

Makamu Mwenyekiti TAIFA: 
Ndugu zangu watanzania habari za jioni, leo ni siku muhimu sana siku ambayo ACT Wazalendo kinafungua kampeni,tumekuja kuanzia Mbagala tukija kuamini kuwa watu wa hapa wanaijua nchi yao,wana machungu na nchi yao hivyo watawakilisha watu walio wengi.

Kila kabila lipo Dar,usije ukadanganyika kwa barabara nzuri, au maisha mazuri ya Dar, usije thubutu kupiga kura kwa kudanganyika na hivi bali piga kura kwa kumsaidia aliye kijijini anayeteseka.

Waangalieni wagombea wetu hususani wa urais, Mgombea wetu naamini ni mgombea makini kuliko wote.Hana shutuma nyingi, wengine wamebaki wakigombanamara fisadi, wezi, wachafu lakini mama Anna pekee ndio huwezi kusikia akiwa na kashfa wala madoa yoyote.

Tunafungua leo kampeni tukiamini mtu tunayemleta kwenu ni mtu safi,makini na asiye na madoa.Naamini watu wa Dar leo mtaonesha kupiga kura kwa kuwasaidia wengine walio Vijijini.

Mkutano nimeufungua Rasmi...
Wananchi wanaimba Wimbo wa Taifa...

Katibu Mkuu wa Chama - Samson Mwigamba; UTAMBULISHO

Dar es Salaam oyeee, ACT-Wazalendoooo....
Ndugu zangu wa Mbagala,Dar na watanzaniana wanaotutizama, leo ni siku rasmi ya kufungua kampeni za uchaguzi kwa chama chetu, naomba kuwatambulisha wageni waliopo

- Wagombea udiwani Kata zote za Dar
- Wagombea Ubunge majimbo kumi mkoa wa dar
- Anamtambulisha jaji Mstaafu
- Kansa Mbarouk
- Chambuso
- Washauri wa Chama
- Habibu Mchange
- Naibu katibu mkuu Bara
- Mgombea Urais kutokea Zanzibar
- Mgombea mwenza (Makamu wa rais)
- Makamu wa chama- ACT wazalendo
- Kiongozi wa Chama (Zitto Kabwe)
- Wawakilishi kutoka Kanda mbalimbali waliokuja kuwakilisha kanda zao
1. Kutoka kanda ya Kaskazini (

2. Kanda ya Magharibi (George Patrick) Mgombea mdogo Tanzania mwenye umri mdogo anatokea chama cha ACT, ana miaka 21, Hii inaonesha kuwa chama hiki kinajali vijana kwa ajili ya mabadiliko. Chama cha ACT ndio chama pekee kinachoweza kusimamia ilani za vijana,ndio kinajua kuwa vijana wafanye nini.

3. Modestus Kiluvi (Nyanda za juu kusini) Watanzania hawa ukiwanyima haki wataitafuta haki kwenye vyama vingine.kwa mara ya kwanza nilipojiunga na chama tulipelekwa kwenye mafunzo hivyo hatuenzi kkuzungumza mambo yetu.Watanzania wanataka haki,wanataka maisha mazuri.Maendeleo hayaji bili kufanya mabadiliko.ACT ndio chama pekee chenye ilani ya msingi chini ya mama yetu Anna.

4. Eva Mpagama (Kanda ya kati) Mbunge wa jimbo la Ikulu Ndogo (Dodoma) ambalo limepoteza Hadhi. ACT ndio chama pekee kilichowaunganisha wakina mama kwa asilimia 25. Ni chama pekee tokea uhuru ambacho kimesimamisha mgombea urais Mwanamke.Ni chama kinachojali nguvu na juhudi ya akina mama.

5. Mama Sijaona (Kanda ya Kusini - mgombea wa Newala) Nikiwa nimezaliwa na baba mhasisi wa tanu,miaka yote baada ya kuona mambo hayako sawa niliamua kukaa pembeni mpaka hapa nilipoona

6. Mustafa Akunaay ( Mwakilishi Wazee na mgombea wa ubunge Mbulu) Chama chetu kinaleta kampeni isiyotumia pesa,isiyotumia matusi. Tunaleta siasa zitakazotekeleza maendeleo.Sikilizeni ilani za chama,gharama za chama.Ukimchagua rais ambaye atatumia magari mengi kwenye msafara ujue gharama zote zitalipwa baada ya uchaguzi,ila ukimchagua mgimbea mwege magari machache kama wetu basi gharama hizo haziwezi kuwa kubwa.Madiwani wetu watafanya kampeni nyumba kwa nyumba hivyo gharama zitakuwa ndogo

7. Janeth Joel (Mgimbea jimbo la Kawe - Mwakilishi wabunge wa Dar) ACT tunakuja na fikra mpya kwenu, watz hawataki kuyumbishwa ila wanataka kusikia fikra pevu, na hayo yote watayapata Act wazalendo.

8 Elia Msoke (Mwakilishi wa walemavu) chama cha kizalendo na chama kinachojali watanzania.Nafasi hii sijapewa bure,naiweza na naimudu.Nawaambia walemavu wote kuwa mwakilishi wenu nitawawakilsha vyema.Tokea mwaka 1961 walemavu hawajawahi kpata uwakilishi mzuri.juzi mlemavu mmoja juzi alisimama na kutaja sera za uongo kwasababu yeye ana mapenzi na chama hicho ambacho sitokitaja jina.Nimalizie kwa kuwaomba Anna,Zitto nawaomba,nna shauku,hizi dakika nilizopewa ni chache,nna madini ambayo nataka niyatoe lakini kwakuwa huu ni ufunguzi naomba mnitumie kwenye kampeni ili nikatoe madini,mimi ni mwanasheria nna uwezo na najiamini.

Mwisho naomba dakika ili nimuombee mama yangu mzazi,mama yangu ambaye amenisimesha pamoja na ulemavu wangu huu mpaka nimefikia hapa nilipo. Namuombea mama yangu ambaye nimemzika jana, hata jana nilikuwa nna safari ya kwenda Bukoba kupeleka msiba lakini baada ya kupata mwaliko wa ACT basi nikaona nibaki, naomba nusu dakika nimuombee mama yangu mzazi


Mshehereshaji anawakaribisha viongozi wa CHAMA

Mshauri wa Chama - Prof. Kitila Mkumbo

Jana nimesikia mtu mmoja anasema kuwa eti urais ni kama meneja.Kwa taaluma niliyonayo naomba niwaambie kazi za rais.

Hapa hatutafuti watu wa kusimamia miradi, hatutafuti watu wa kuzibua mitaro ila tunatafuta rais wa kutoa dira

Kazi za Rais
1. FIKRA - Rais ndiye anayepaswa kutoa dira ya nchi,ili aweze kutoa dira lazma awe na fikra.Hawa mnaowasikiliza muwapime hapa.Huyo anayekuja na kusema nikiwa rais nitaleta maji huyo ni muongo labda kama atakuwa afsa mradi maji

Rais atakayekuja na ukamuuliza atakufanyia nini akasema ngoja nikasome ilani huyo wa kumuogopa ni muongo.

2. Rais ndiye mlinzi mkuu wa Tunu za TAIFA
Kuna tunu mbalimbali lakini za msingi ambazo ni...
- Mlinzi wa Umoja wa Taifa
- Mlinzi wa usawa katika taifa
- Muungano
- Uadilifu
- Demokrasia

3. Lazima awe mfano bora wa binadamu tunayemtaka katika jamii.
Rais tunayemtaka lazma aweze kuwawakilisha watanzania hata huko

4. Muadilifu, rais wetu lazma atokee chama cha kisiasa na ili awe muadilifu lazma chama anachotoka lazma kiwe na uadilifu.Rais anayetoka chama cha kilaghai,chama kinachotaka mafanikio ya haraka huyo hafai.Kama anatoka chama cha kilaghai basi naye atakuwa Laghai.

Uchaguzi huu utakuwa uchaguzi wa Mbwembwe,ulaghai au unachagua misingi na sera, vyama vingine vinauza mbwembwe na ulaghai,sisi tunauza Misingi na Sera.

Habibu Mchange -Meneja Kampeni
Nimetumwa na chama kusimamia kampeni za mgombea wa Urais. Nitaanzia alipoishia Prof. Mkumbo

Angalia kushoto na kulia angalia ni bendera ngapi zinapepea.Alipoishia Mkumbo kuwa kuna vyama via mbwembwe na Ulaghai lakini ukitaka Sera zaipo ACT wazalendo.

Ninyi wakazi wa Temeke na Mbagala Taifa zima linawatizama, 2007 watanzania wa vyama vya upinzani walikutana Mwembeyanga walisema taifa limefika hapa kwasababu watawala wameshindwa kututawala(Alikuwepo mbowe,zitto,slaa,Sharrif) hakukuwepo ukawa na siku ile ilitajwa list ya watu wanaoihujumu nchi.

Katika watu wale 11, document iliyosainiwa na mbowe,lipumba na Mrema mmojawapo alikuwa Lowassa akiwa namba 9. msinipigie makofi ila jitafakari. Mkumbo kasema uliyoyasema jana ndio uyaishi leo.

Kuna rafiki yangu kantumia sms ikisema kuwa nimetumiwa chupa mbili,moja imendikwa maji na nyingine sumu.Sisi ACT tunakuja katikati ya chupa mbili za sumu yaani uKAWA na CCM.

Leo mgombea wa CCM anashangaa kila kitu,anashangaa twiga anapanda ndege,sehemu kuna ziwa lakini hakuna maji. Mgombea wa CCM aache kutufanya watanzania hatujielewi.Shida ya maji,mikopo ya wanafunzi na wakina mama hospitalini zimesababishwa na CCM.Magufuli akija kwa watanzania mwambie aache kutu-enjoy.

Niseme nisiseme? Jana Sumaye , anashangaa kwanini CCM imeendelea kutulaghai.Mwaka 1995 akiwa waziri mkuu na wakati wa ununuzi wa ndege ya Rais tulipoambiwa kura nyasi lakini ndege inunuliwe, Sumaye alikuwa boss. Mauaji ya mwembechai Sumaye alikuwa waziri Mkuu.

Hatuwezi kuendelea kudanganya na CCM na Ukawa,taratibu za Uchaguzi.... Wanasema wakati wa EPA,RICHMOND nani alikuwa waziri mkuu?

Kumbe Tanzania Ukiwa CCM ukawaibia watanzania unakuwa Fisadi lakini Ukihamia Upinzani unakuwa Mtakatifu. Tupinge hii hujuma.

UKAWA wanatudanganya UKAWA UKAWA,kumbe ukawa wanatafuta Urais lakini huku chini kwa wapiga kura UKAWA hakuna.

Tabora mjini wakati CHADEMA wameweka mgombea wao,CUF na NCCR nao pia wameweka wagombea sasa Lowassa akienda Tabora ataomba kura kwa mbunge gani?

UKAWA mpango wao ni kushika dola bila hata bila wabunge, ila chama cha ACT wazalendo tumejiandaa kushika dola.Na viti vya wabunge tanzania nzima ACT wazalendo imesimamisha wagombea kwenye majimbo yote,cha pili ni CCM na Cha Tatu ni CHADEMA.

Nimekuja kwenu mtuunge mkono,mtuchagulie rais,wabunge na madiwani wa ACT wazalendo ili twende IKULU tukafanye kazi.CCM imeshindwa kuwatumikia watanzania.

ACT wazalendo utaifa kwanza.... UFISADI mwisho UKAWA na CCM.

Naomba sana Kiongozi wa CHAMI,Mwami Zuberi Zitto aje hapa,hadhara hii ipo tayari kusikiliza ACT wazalendo


Kiongozi wa Chama - Mwami Zitto Kabwe
Nampongeza kampeni meneja kwa maneno yake yanayotofautisha kati ya washindani na wenye nia

Naona kuna sehemu moja amezidiwa na kuongelea ugonjwa, naomba nichukue nafasi hii kwa niamba kuomba msamaha.

Mimi leo sio siku yangu ila ni siku ya mama Anna. Kampezi zetu ni UTU,UZALENDO na UADILIFU (Anaelezea kipengele kimoja kimoja)

Kila chama kinachogombea kimesema kitapambana na rushwa na ufisadi lakini hawajasema watapambana vipi, ACT Wazalendo pekee ndio kimesema kitapambana kwa kurejesha MIIKO na UADILIFU.

Nchii hii imeongozwa na mawazili wakuu wengi na mpaka sasa watatu wametangulia mbale ya haki ambao ni mwalimu Nyerere, Sokoine na Kawawa.... Mawaziri wakuu wanne wako CCM, Sumaye na Lowassa wako Ukawa na Malecela hajataja upande wake.

Hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kurudisha watu wale wale ambao walituletea kadhia kwenye nchi.

Chama chenye uwezo wa kuleta mabadiliko (Changes with Content) ni ACT wazalendo pekee ndio maana tumewaletea mama. Nchii hii imeongozwa na marais wanne na kumekuwepo na ufisadi wa kutisha, ACT wazalendo tumewaletea mama ili aweze kukabiliana na ufisadi huu.

Wagombea waliopita wamesema watatoa baadhi ya huduma bure kama elimu, lakini hawatuambii pesa watatoa wapi hizo pesa za kuendesha elimu bure.

CCM wamesema watatoa 50ml kwa kila kijiji ambazo ni pesa nyingi,lakini hawajasema watatoa wapi hizo pesa kama sio kuwabebesha wananchi mzigo wa kodi.

Nchi yetu inapoteza kodi zaidi ya bilioni 600 kila mwaka kwasababu baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kodi.Sio CCM wala UKAWA wanaweza kuwataja maana ndio wafadhili wao wakubwa wa kampeni.

ACT wazalendo mkimpitisha mama msiulize tutapata wapi hela za kutoa huduma hizo, mama ataziba mianya yote ya Rushwa na pesa zitapatikana na kuwekezwa kwenye miradi.

Tunaambiwa ufisadi sio ajenda,wakati huu wa kampeni kuna watu wanaendelea kupiga pesa, juzi hapa kuna kampuni kutoka Switzeland kuna kampuni imepewa tenda na tenda ile haikutangazwa, katika tenda hiyo wapigaji watapata zaidi ya bilioni 20. Chagueni ACT wazalendo ili ajenda ya Ufisadi tuweze kuisimamia

Kwenye ilani yeti tumesisitiza uzalendo,tumesisitiza tutawafanyia nini watanzania.Mgombea na mgombea mwenza watakuja kueleza ndani ya muda mchache ujao.

Tarehe 5 mwezi ujao, timu yetu ya taifa itacheza na timu ya Nijeria,nawaomba TFF wawaruhusu wananchi wakaishangilie timu yao bure. Mipango yetu ni kuhakikisha kuwa timu ya Taifa inacheza kombe la dunia.

Magufuli mlishawahi kumuona Taifa, mtu kama huyo kweli anaweza kukuza michezo? ACT wazalendo ndio pekee tunaweza kukuza michezo na ndio maana nawaambia Jumamosi wote tukutane Uwanja wa Taifa Tukaishabikie timu ya Taifa ili ishinde na kuingia hatua ya pili.

Zitto anawakaribisha wagombea wa Ubunge kwa mkoa wa Dar wajitambulishe
- Anaongea aliyekuwa mbunge wa Kigamboni ambaye kahamia ACT na anagombea Jimbo la Rungwe.
- Anaongea mgombea wa Ubunge wa Mbagala
- Anaongea Kalapina ( Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni) - Muuza Unga wa Kinondoni Ananiogopa
- Anaongea Mgombea wa Jimbo la Ubungo
- Anaongea Mgombea ubunge jimbo la Ukonga ( kwa mbwembwe anampa onyo Jerry Silaa)
- Anaongea Mohamed Mwikongi wa Jimbo la Segerea
- Anaongea mgombea wa jimbo la Temeke - Wanatemeke wamenituma kuwa wamekosa mwakilishi makini miaka yote, Mtemvu amesikika akitetea kuhusu ESCROW na mara ya pili kuhusu mwanaye kuvuliwa taji la miss Tanzania
- Anaongea wa Kigamboni
- Anaongea wa Jimbo la Kawe
- Anaongea wa Jimbo la Kibamba
- Anaongea wa jimbo la Ilala

Seleman Msindi (Afande Sele)

Siku mkiona naapishwa kuwa mbunge basi kila mmoja aseme kuwa Chizi kalogwa tena, sasa nawakaribisha mgombea urais na Mgombea mwenza

Mgombea mwenza - Hamid Yussuf
Nnayo hekima kubwa kusimama mbele yenu,namshukuru Mngu kunipa hekima hii, nawashukuru viongozi wa Chama na wanachama kwa kuniamini na kunipa nafasi hii.Tatu nachukua nafasi hii kuwapa shukrani wazazi wangu ambao wametangulia mbele ya haki.mwisho mke wangu ambaye amenivumilia kipindi chote nawatumikia watanzania.

Miez miwili ijayo naenda kuapishwa kuwa makamu wa rais wa Tanzania na nakwenda kufanya kazi,siendi kuwa mzibua mitaro.

Kuna wagombea wanaogopa mabadiliko lakini napenda kuwahakikishia kuwa yaliyotokea Tunisia ni pale kijana aliyemaliza masomo yake baada ya kukosa ajira akajiajiri lakini alikamatwa na manispaa ndio akajimwagia mafuta na kujichoma na ndipo mabadiliko yalioanzia na mpaka sasa mambo shwari.

Sitaki yatokee mabadiliko kama Tunisia ila sisi mabadiliko yetu yawe kwenye boksi la kura ili act wazalendo tuweze kuingia ikulu na kuwatumikia watanzania.

Mgombea Urais - Anna Mghwira

Anawashukuru watanzania

Nasimama mbele yenu kuomba ridhaa kwenu watanzania ili niweze kuwa rais wenu.Watanzania ni sehemu ya vijana na wazee,wanawake na waume 

Mkinipa ridhaa nitaunda serikali umoja itakayotokana na viongozi wazalendo,waadilifu watu kutoka sekta binafsi ila wawe waadilifu,wazalendo ili kuunda taswira ya nchi yetu.

Kwenye kujenga Taifa hakuna hitakadi ya udini wala jinsia bali utaifa.

Serikali yetu ikiundwa italeta vipaumbele vyake mapema, serikali yetu itahamishiwa Dodoma na sio makao makuu ya Chama.Tutaamua makao makuu ya Chama yawe mkoa gani.

Dodoma maana yake ni kuwaletea umoja wananchi wetu.Chama chetu kimeweka na mimi natasimamia ili kufanikisha.

Chama chetu kimekuja na vipaumbele vikuu vinne...

1. Hifadhi ya Jamii
2. Uchumi shirikishi na wenye kuzalisha ajira nyingi na bora. Baada ya kuingia madarakani tutaruhusu tume ya Warioba imalizie mchakato
3. Afya, Tanzania ina mfumo mbaya wa huduma za afya, chini ya ACT itahakikisha kila mtanzania anafahamika alipo na huduma zinamfika.
4. Elimu, watoto wanamaliza shule hawajui kusoma na kuandika, mwanafunzi wa chuo kikuu anashindwa kujieleza, ACT tutajitahidi kunua vipaji, leo tumezalisha watoto wa mitaani.

12:04 jioni - Mama amemaliza Hotuba yake.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto (kushoto), akiteta jambo na  Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.
 Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.
  Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.
 Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.
Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post