REDDS MISS TANZANIA 2015 NA MISS KENYA WATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT KUWAFARIJI WAGONGWA

 Miss Kenya, Idah Nguma.
 Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima.
 Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima (kushoto), akiwa na Miss Kenya, Idah Nguma baada ya kuwatembea wagonjwa katika hospitali hiyo.
 Mmoja wa Maofisa kutoka Taasisi ya Smile Train inayofanya kazi na Miss Kenya, Idah Nguma, Jane Ngige akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima (kulia) na Miss Kenya,  Idah Nguma (kushoto), wakiwa na mmoja wa wadau wa Hospitali ya CCBR iliyopo Msasani, baada ya kufanya ziara ya siku moja katika hospitali hiyo ya kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kuona huduma mbalimbali zinazotolewa hospitali hapo Dar es Salaam leo asubuhi. Miss Kenya, Idah Nguma yupo katika mfululizo wa ziara ya kutembelea hospitali zinazotoa matibabu ya mdomo wazi na vistula.

Na Dotto Mwaibale

MISS Kenya Idah Nguma ametembelea nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea Hospitali ya CCBRT kuwafariji wagonjwa pamoja na kuona  huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.

Katika ziara ya kutembelea hospitali hiyo Nguma aliongoza na mwenyeji wake Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima na mmoja wa maofisa wa kamati ya kuratibu Miss Tanzania.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo  Dar es Salaam leo asubuhi ,Nguma  alisema amefurahi kuja nchini hapa  kwa mara ya kwanza huku lengo lake likiwa ni kuangalia mradi wa Smile Train ambao upo swizland. 

Nguma alisema mradi huo ni wakusaidia wanawake wenye festula pamoja na watu wenye matatizo ya mdomo wazi. 

"Mimi ni Balozi  katika shirika hilo na nimekuja kuangalia huduma kwa wagonjwa wa Fistula na Midomo wazi (sungura)" alisema Nguma.

Nguma alisema  amefurahishwa na huduma inayotolewa  na wahudumu waliopo katika hospitali hiyo pia atakapofika katika ziara yake ya kwa nchi ya Uganda atawaelimisha  jamii na wananchi wa Uganda kwa huduma bora wanyopata watu wenye matatizo hayo. 

Pia hata Miss wa Tanzania Lilian Kamazima amesema kuwa wamemkaribisha kwa furaha Miss wa Kenya hiyo yote ni kudumisha amani na upendo katika nchi hizi mbili.

Alisema  ziara yake ya  kuwaona wagonjwa ni moja ya kuonyesha kuwajali wagonjwa  na kudumisha upendo na kuwapatia faraja na kuowaongezea matumaini ya kuona kuwa na wao ni miongoni mwa watu katika jamii.

"Nimefurahishwa na huduma inayotolewa katika hospitali hiyo hasa baada ya  kuona wagonjwa wanaendelewa vizuri""alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Post a Comment

Previous Post Next Post