Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Uongozi wa Kampuni ya Tanzanite One ya wilayani Simanjiro Mkoani Manyara umesema kuwa Mbunge wa jimbo la Simanjiro ,James Ole Millya amelipotosha bunge na umma kwa ujumla kwa kusema kauli ambazo hakuzifanyia utafiti wa kina.
Millya katika kikao cha Juzi bungeni alisema kuwa kampuni ya Sky Group Associates iliyonunua hisa kwa kampuni ya Tanzanite One na kumiliki kitalu C cha madini ya Tanzanite Mererani wilayani humo hakikufuata taratibu za ununuaji wa hisa hizo na kuwatuhumu baadhi ya Mawaziri kuwa walihusika katika kupindisha taratibu.
Mbali ya hilo Mbunge huyo alienda mbali zaidi na kuituhumu kampuni hiyo kwa kuwafukuza kazi wafanyakazi 201 bila ya kufuata utaratibu na kuwa kampuni ya Tanzanite One inanyanyasa wafanyakazi.
Akizungumza kwa njia ya simu mwanasheria wa kampuni hiyo,Kisaka Mzava alisema uongozi wa Tanmzanite One umesikitishwa na kauli ya Mbunge Millya aliyesomea taaluma ya sheria kwa kusema vitu ambavyo hafanyia utafiti wa kina hatua ambayo uongozi unashaka na taaluma yake kwani vitu kama hivyo hata mtoto mdogo hawezi kusema.
Mzava alisema na kumtaka mbunge huyo kwanza kujilidhisha kwa kufanya utafiti wa kina namna hisa za Tanzanite One zilizouzwa kwa kampuni ya Sky Group inayomilikiwa na wazawa kwa asilimia mia na wamiliki wa hisa wanajulikana na kama anahitaji kujuwa anapaswa kwenda Brella kujilidhisha.
Alisema hakuna Waziri wala kiongozi yoyote mwingine wa serikali anayemiliki hisa katika kampuni hiyo na kulichosemwa na Mbunge Millya kinapaswa kulaaniwa.
Mwansheria huyo alisema Sky Group katika ununuzi wa hisa hizo umeshalipa kodi ya serikali yote bila ya wasiwasi na kampuni hiyo sio kampuni ya mfukoni kama anavyodai kwani mbunge huyo amelipotosha bunge na umma kwa ujumla kwa maslahi yake binafsi.
Mwanasheria huyo alisema shughuli za uzalishaji zinasimamiwa kikamilifu kati ya kampuni ya Sky Group na serikali kupitia Stamico na hakuna madini yanayoibiwa kama Mbunge huyo anavyosema na kama ana ushahidi wa wizi huo anapaswa kuutoa nje ya bunge.
Alisema hakuna njia ya mkato iliyofanywa katika ununuwaji wa hisa na hakuna Waziri yoyote aliyehusika katika kusaidia kupindisha taratibu kwani kila kitu kipo wazi na alichosema mbunge Millya anapaswa kukitolea ushahidi nje ya bunge na sio ndani ya bunge.
Akizungumzia kufukuzwa kwa wafanyakazi,mwanasheria huyo alisema kuwa wafanyakazi 201 waliofukuzwa kazi ni wafanyakazi hatari kwa mstakabali wa kampuni kwani ni wachochezi,na wenye hila za kutaka kuihujumu kampuni hiyo ili iweze kuleta maafa.
Mwanasheria huyo alisema kugoma ni kosa kisheria kama mgomo hakufuata taratibu sheria lazima zichukue taratibu na ndio uongozi wa Tanzanite One umechukua kwa kuwafukuza kazi wafanyakazi hao 201 walipogoma bila ya kufuata taratibu.
‘’Sheria za kazi ziko wazi kugoma,kuhujumu kampuni na kuchochea wafanyakazi kugoma na kuhujumu kampuni ni kosa kisheria hivyo uongozi wa kampuni haukusita kuwachukulia hatua kwa hilo’’
‘’Wafanyakazi waliofukuzwa kazi walistahili kufukuzwa na kama kampuni ilikiuka taratibu sheria iko na vyombo vya kisheria viko na siasa isiingizwe katika masuala ya kisheria’’
Mwanasheria huyo alisema Waziri wa Nchi,ofisi ya Waziri Mkuu sera,Bunge,kazi ajira vijana na walemavu Jenista Mhagama hana ndugu na mtu anayefanya kazi katika kampuni ya Tanzanite One na kilichosemwa na Mbunge Millya ni kukurupuka na uongo wa kupindukia ambao haukufanyiwa utafiti wa kina.
Mzava alisema Nasibu Mhagama ana mtoto anaitwa Yufuph Mhagama ambaye anafanya kazi Tanzanite One na hawana uhusiano wowote na Waziri Mhagama na wala hawamujii.
‘’ Yusuph Mhagama ni mtoto wa Nasibu Mhagama hawana uhusiano wowte na waziri Jenista Mhagama na wala hawamjui’’ Mwanasheria huyo
Kampuni imesikitishwa sana na upotoshwaji ulitolewa ndani ya bunge na mbunge Millya na inashaka na taaluma ya sheria ya mbunge huyo kwani hakufanyia utafiti hoja aliziwasilisha bungeni na kuonekana kutumika kwa maslahi yao watu wengine.
Post a Comment