TIKETI ZA BAHATI NASIBU YA TAIFA ZAANZA KUUZWA

Mwenyekiti wa kampuni ya  Gidani  ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Profesa Bongani Aug Khumalo,akitoa maelekezo ya mchezo huo kwa waandfishi wa habari na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi, (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba  na katikati ni Meneja mradi wa  Kampuni hiyo,Brett Smith.
Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya  Michezo ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akijaribu mashine za michezo zinavyofanya kazi
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Gidani wakisikiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha,Abbas Tarimba (hayuko pichani) muda mfupi baada ya hafla ya  uzinduzi wa kuuza tiketi.
……………………………………………………………………………………………………..
-Mshindi wa kitita cha milioni 100 kujulikana Jumamosi
Kampuni ya Murhandziwa Limited ya Afrika ya Kusini ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa leo imeanza kuuza tiketi nchini kote na droo ya kwanza ya mchezo huo itafanyika jumamosi ya wiki ijayo  ambayo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 100.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kuuza tiketi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania,Abbas Tarimba amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kushiriki  bahati nasibu inayoendeshwa kitaalamu na inayowezesha  washindi kujishindia donge nono  na kubadilisha maisha yao.
“Zawadi ya milioni 100 sio  ndogo  itasaidia kubadilisha maisha ya mshindi pia zitatolewa zawadi mbalimbali na serikali inategemea kupata mapato kwa njia ya kodi Zaidi ya dola milioni 40 kwa mwaka kutokana na uwekezaji huu katika sekta hii na aliwataka watanzania wachangamkie kununua tiketi na kushiriki katika mchezo huu.
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandizwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo alisema kuwa watanzania wategemee kuona michezo ya kubahatisha ikiendeshwa kitaalamu na kubadilisha maisha ya washindi kutokana na zawadi nono watakazopata washindi.
“Tiketi za Bahati nasibu hii zitauzwa kwa shilingi 500 na zitapatikana kwa mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washitiki wa mchezo huu wa Bahati Nasibu ya Taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,vilevile droo nyingine za mchezo zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi na kuwezesha wananchi wengi kushinda”Alisema.
Alisema mbali  na mchezo huu kuwanufaisha washindi binafsi utawawezesha watanzania wengi kupata ajira Zaidi ya 1,000 za moja kwa moja na zisijo za moja kwa moja ambapomkwa sasa imeajiri watanzania 40 na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kuwa imeajiri wafanyakazi Zaidi ya 1,000.

Post a Comment

Previous Post Next Post