Shule ilimuomba msamaha mwanafunzi na mamayake
Shule moja katika jimbo la California nchini Marekani imeamrishwa kumlipa dola 1.25 mwanafunzi wa zamani ambaye alienda haja ndogo kwenye ndoo baada ya kunyimwa nafasi ya kuenda chooni.
Jaji alitoa uamauzi huo kufuati kesi ambapo shule na mwalimu walishtakiwa kufuatia kisa hicho kilichotokea mwaka 2012.
Shule ilisema kuwa mwalimu hakuwa na nia ya kumkosea heshima mwanafunzi.
Mawakili wa shule walisema kuwa mwalimu alijaribu kutafuta suluhu, kwa kile alichofikiri kuwa sheria kali za wanafunzi kutopewa ruhusa ya kuenda chooni wakati wa masomo.
Mwanafunzi huyo wa shule ya Patrick Henry High School, ambaye sasa ana umri wa miaka 19, anasema kuwa mwalimu Gonja Wolf alikataa ombi lake la kutaka kuruhusiwa kuenda chooni.
Bi Wolf badala yake, alimuamrisha mwanafunzi kutumia chumba kilichokuwa kando ambapo alikojoa kwa ndoo.
"Kisa kama hiki kamwe hakingemfanyikia mwanafunzi wa umri wa miaka 14 ambaye alikuwa amejiunga na shule ya sekondani," wakili wa mwanafunzi alisema.
Kando na dola milioni 1.25, jaji pia aliamrisha mwanafunzi huyo kulipwa dola 41,000 kwa huduma za matibabu.
Mwalimu alipewa likizo na hakurudi shuleni humo baada ya kisa hicho.
Shule ilimuomba msamaha mwanafunzi na mamayake na kuwaeleza walimu kuwa nafasi za kuenda chooni zimeruhusiwa.
Chanzo: BBC Swahil.
Post a Comment