Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amesema kuwa Mkoa hauna njaa baada ya kufanya ziara katika maghala mbalimbali ya wajasiriamali pamoja na kiwanda cha Unga cha Energy Mills vyote vilivyopo katika mji wa Sumbawanga.
“Mmejionea wenyewe, Katika Manispaa ya Sumbawanga suala la kwamba hakuna chakula ama kuna njaa ni maneno hewa, hakuna kitu kama hicho, Chakula kipo cha kutosha nafaka karibu zote zipo,” Mkuu wa Mkoa alisisitiza.
Ameongeza kuwa wakulima wengi wameonekana kuuza mazo yao kwa wachuuzi na kusababisha wafanyabiashara wa masokoni kwenda kununua mazao hayo kwa bei na matokeo yake naoi li wapate faida nao wanaongeza bei jambo linalosababisha wananchi kushindwa kununua na wao kulalamika kuwa hakuna wateja.
Katika suala la malalamiko ya wananchi kuosa pesa Zelote Stephen alifafanua “malalamiko yaliyokuwepo kuwa pesa hakuna, nami nakubali, kipindi hiki tulichopo ni wakati wa kilimo na wakati wa kilimo maana yake kila mtu yupo shambani, na mwezi ujao (Februari) kuanzia tarehe 20, kuna taarifa kwamba watu wataanza kuvuna maharage, kwahiyo ni dhahiri kwamba suala la njaa na bei hakuna mtu ambae atalizungumzia.”
Katika kulishuhudia hilo mmiliki wa kiwanda cha Energy Mills, Aziz Tawakali alisema kuwa mpaka sasa katika ghala lake ana tani 30 na mifuko 3400 ya unga wa sembe wenye kilo 50 kwa kila mfuko, na kuongeza kuwa kwa idadi hiyo kiwanda chake kinaweza kufanya biashara hadi mwezi wa tatu mwaka huu.
“Sio kwamba kuna njaa, na katika mwaka mzima hatujawahi kukosa stock ya chakula, na wa stock hii niliyonayo nina uwezo wa kuuza mpaka mwezi wa tatu” Azizi alithibitisha.
Nae mmoja wa wamiliki wa mashine za mpunga Mathias James amethibitisha kuwa katika Mkoa wa Rukwa hakuna shida ya chakula bali shida iliyopo ni ya wateja wa kununua chakula hicho, hivyo aliwaasa wale wote wanaosema kuwa hawana chakula cha kununua wafike katika ofisi yake.
“Kusema kuwa kuna njaa, hiyo si kweli, maana sisi tunahangaika kutafuta wateja, na wateja tunaowategemea ni kutoka Mbeya na Tunduma na wengine kutoka nchi za jirani kama Zambia na Kongo, hivyo tunawaasa wale wanaotafuta mchele, kwetu upo, tuna magunia ya mpungaya kilo 90 zaidi ya 18,000 hayana wateja, mpunga upo, mahindi yapo, waohitaji watuone,” Mathias alisisitiza.
Nao baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo wanouza kwa visado nao pia waliendelea kulalamikia upungufu wa fedha katika mifuko yao na kuongeza kuwa shida za wananchi si chakula kwa sasa bali pesa ndio ngumu na ndio inayotusababishia njaa.
“Njaa yetu pesa hakuna chakula kipo ila hela ya kununulia hayo mahindi ndio hakuna, kutokana na mzunguko wa biashara hela hakuna ila chakula kipo,” Deus Malonga alisema.
Nae Agness Palakata alisema “Tokea asubuhi tunauza hilo gunia halijaisha, sasa namna hii hatuwezi kurudi nyumbani uawalisha watoto, pesa hakuna, chakula kipo ila pesa ndio tatizo, shida yetu na njaa yetu ni pesa.”
Kwa kuthibitisha kutokuwepo kwa njaa Zelote Stephen aliongeza kuwa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wana jumla ya tani 15,500 ambazo zipo kwenye magala yao.
Kaimu Afisa Habari Mkoa wa Rukwa
Abdulrahman Salim.
17/01/2017.
Post a Comment