ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII

Vyombo vya habari nchini hususani redio za kijamii zimetakiwa kuandika habari ambazo zinaelezea changamoto ambazo zinawakabili wananchi katika maisha yao ya kila siku na jinsi ambavyo wanaweza kuzitatua.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.
Alisema wanahabari na vyombo vya habari ni muhimu nchini kwa maendeleo ya Taifa lakini kama wasipokuwa makini katika utendaji wao wa kazi kunaweza kuwa na madhara makubwa hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa habari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa kwanza kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

Alisema sehemu kubwa ya wananchi ambao wanaishi vijijini hawapati taarifa muhimu zinazohusu maendeleo yao zikiwepo taarifa za kilimo, afya, mazingira na haki za kibadamu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanaandika habari ambazo wananchi wamekuwa hawazipati kwa muda mrefu.

“Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha redio hizo zinatimiza malengo yake hususani katika kumuelimisha wanajamii, kuwajengea uwezo wa kutambua na kupambana na mazingira ili kuinua hali zao za kimaisha,” Mhe. alisema Wambura.

Alisema mafunzo hiyo ni muhimu kwao kama wawakilishi wa redio za kijamii sababu itawapa mbinu ambazo wanaweza kuzitumia ili waweze kujisimamia wao wenyewe bila kuwa tegemezi kwa kuomba fedha kutoka sehemu zingine.


Picha juu na chini ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akisoma hotuba ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

“Natambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa redio za kijamii ambazo ni kama upatikanji wa habari endelevu na zinazolingana na mahitaji ya jamii husika, uhaba wa rasilimali fedha za kuendeshea redio husika, na udhaifu katika usimamizi stahiki wa taasisi hizo lakini kwa hakika mafunzo haya ni muhimu kwa vile yanalenga kutatua changamoto hizo,” alisema Wambura.
Aidha Naibu Waziri Wambura amewashukuru Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kujenga Taifa lenye waandishi na wasimamizi wa habari wenye weledi na kazi zao pia mafunzo hayo yanakwenda sambamba na dira ya wizara ya kuwa na Taifa lililohabarishwa vizuri ifikapo 2025
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida amesema mafunzo hayo yamekuja baada ya kufanyika utafiti mwaka 2014 kwa ufadhili wa UNDP, utafiti ambao ulifanyika kwenye wilaya tano nchini na kugundua kuwa njia bora ya upashaji habari katika maeneo hayo ni kwa kutumia redio.
Amesema baada ya matokeo hayo ya utafiti walipendekeza kuanzishwa kwa redio jamii katika maeneo ambayo utafiti ulifanyika ili kurahisisha taarifa mbalimbali za kuelimisha wananchi ambazo zitakuwa chachu kubwa ya maendeleo kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

“ESRF kwa ufadhili wa UNDP ilisimamia uanzishwaji wa redio jamii nne ambazo ni Redio Unyanja (Nyasa), Redio Bunda (Bunda), Redio Kagera (Bukoba Vijijini) na Redio Ileje (Ileje) na redio zingine mbili Redio Sengerema (Sengerema) na Redio Mazingira (Bunda) zilipata misaada mbalimbali kwa ajili ya kujiendesha,” alisema Dk. Kida.
Mafunzo hayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii kutoka wilaya tano nchini ambazo ni Ileje, Bukoba Vijijini, Bunda, Nyasa na Sengerema pamoja na wawakilishi wa halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.


Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akitoa taarifa kwa washiriki wa mafunzo kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC), Dotto Kuhenga akitoa mafunzo kwa washiriki kuhusu redio jamii na jinsi zinavyotakiwa kufanya kazi.
Picha juu na chini ni Mtaalamu wamasuala ya Tehama kutoka ESRF, Joseph Ngonyani akitoa mafunzo kwa washiriki jinsi wanavyoweza kutumia mitandao kuapata taarifa ambazo wanaweza kuzitumia kwenye redio zao.


Washiriki wa mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post