JOKATE AIBUKA KIDEDEA! MASTAA NA MAKE UP, AWAFUNIKA WEMA SEPETU, KAJALA N.K....

Jokate Mwegelo
ILIKUWA safari ndefu ya mtifuano wa hali ya juu kati ya mastaa kibao kwenye shindano hili lililodumu kwa takribani miezi miwili na leo mshindi amepatikana ambaye ni Jokate Mwegelo. Jokate ameibuka kidedea baada ya kupigiwa kura nyingi na wasomaji wakionesha kuwa, yeye alikuwa ni zaidi ya Hamisa Mobeto aliyekuwa akichuana naye.

Shindano hili linafika tamati baada ya kuwashindanisha mastaa kibao wa kike Bongo ambao wamekuwa wakitupia picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ambapo baada ya vuta nikuvute sana, Wema Sepetu, Kajala, Wolper, Tunda, Nisha, Esther Kiama, Zari, Pretty Kind, Hamisa Mobeto na Jokate waliingia 10 bora.
Leo kitendawili kimeteguka! Jokate ndiye kiboko yao. Mwanadada huyo ambaye kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mbali na kujishughulisha na mambo ya ujasiriamali, pia ni mwanamitindo anayeonekana kupambana kuhakikisha anatimiza ndoto zake.

Kuhusu zawadi yake, mdhamini wa shindano hili ambaye ni mmiliki wa Duka la Vipodozi AK Cosmetics amesema, siku yoyote staa huyo akiwa tayari atakabidhiwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post