MODEL WA VIDEO ‘Ntampata Wapi’ YA DIAMOND ASHINDA TAJI LA TOP MODEL NCHINI SOUTH AFRICA

Unamfahamu Melissa Magiera ambaye amewahi kuonekana kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’ ya Diamond? Nadhani utakuwa umeshamkumbuka kupitia video hiyo niliyokutajia.
                                                    Melissa Magiera
Mrembo huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya kampuni ya Fan Jam Model Management, wiki iliyopita amefanikiwa kushinda taji la Top Model 2018 nchini Afrika Kusini.
Melissa ameshinda taji hilo kwa kuwabwaga washiriki wengine 38 ambao walifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali.
Mrembo huyo ataiwakilisha Afrika Kusini kwenye mashindano ya Top Model ya dunia ambayo yatafanyika Ijumaa ya April 6 na 7 ya mwaka huu mjini London.

Post a Comment

Previous Post Next Post