UBUNIFU: MAKEKE AJA NA VAZI LA UNGO LINALOTAMBULIKA KWA JINA LA "LUPAHERO".


LUPAHERO
Baada ya uzoefu mkubwa katika matumizi ya mapishi jikoni, ungo umejizolea umaarufu mkubwa baada ya kuingizwa rasmi katika tasnia yasm sanaa na hususani katika ubunifu wa mavazi na kupewa jina la LUPAHERO na Jocktan Makeke.

Maanaya LUPAHERO

Ubunifu huu wa mavazi umepewa jina la LUPAHERO ambalo ni mchanganyiko wa majina mawili ambayo ni LUPAPIKE, neno la kinyakyusa lenye maana ya ungo na neno la pilini LUHELO, ambalo ni neno la kihehe lenye maana ya ungo.

Muunganiko wa maneno haya mawili yamelenga kuleta dhana ya ushujaa kutokana na ladha ya mavazi hayo kuwa na dhima hiyo, huku neno Luhelo likitamkwa herufi zamwisho kama Hero, herufi L ikibadilishwa kuwa R ilikupata neno hero la kingereza lenyemaana ya shujaa na kukamilisha maana halisi ya ubunifu huo kuwashujaa wa ungo.  

Jinsi wazo lilivyopatikana.

Katika maandalizi yaonyesho la kwanza kufanywa chini ya MAKEKE INTERNATIONAL lililofahamika kama I AM MAKEKE ndipo wazo hili la lupahero lilipozaliwa. Kwamujibuwa MAKEKE INTERNATIONAL ilimchukua muda mrefu kupata wazo la kufanya katika onyesho hilo licha ya kua na bidhaa nyingi za kubuni nguo mbalimbali ofisini kwake.

Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ndani ya ofisi, alitoka nje na kurudi baada ya kutuliza akilila na wakati akirudi aliuona ungo kupitia dirisha uliokua umetundikwa ukutani kama pambo la ofisia mbapo aliamua kuuchukua na kukaa nao huku kichwa kikiendelea kuwaza na kuwazua ni wazo gani ataonyesha kwenye onesho lililokua mbeleyake.

Baada ya kuwaza kwa masaa kadhaa wazo lilimjia na kutaka kutoboa ungo aliokua nao  kwakiasi cha kuweza kuvaa shingoni ambapo alifanya hivyo na kupata ladha ya mapambo ya shingoni ya kimasaii la katika mwonekano wa ungo na ndipo alipoanza kufikiria mikato mingine ambayo   ungo unaweza kuingia na kudhihirisha ubunifu wa ungo kama vazi.

Baada ya kupata yote hayo Makeke alichukua daftari na kuanza kuchora kila alichokua amekiwaza kwa ufanisi zaidi kufanyia kazi kwa muda aliokua nao hali iliyofanya ubunifu wa ungo kutumika kwamara ya kwanza katikatamasha la I AM MAKEKE mpaka hivisasa.

Mikato ya Lupahero

MAKEKE INTERNATIONAL 
imelenga zaidi kujenga dhana ya ushujaa na asili ya kiafrika ili kujenga mazingira ya kuweza kujiamini na kujua kuwa wewe ni bora zaidi kutoka na jinsi ulivyo kama mwafrika na shujaa akiwa katika kila jambo.
Follow us on Facebook  @makeke international Instagram@makekeinternational  

Post a Comment

Previous Post Next Post