Mshukiwa Nguli wa utekaji nyara nchini Msumbiji akamatwa huko Afrika Kusini


Mwanamume mmoja raia wa Msumbiji anayetuhumiwa kupanga utekaji nyara kwa lengo la kutaka kukomboa fedha amekamatwa na polisi wa kimataifa wa Interpol nchini Afrika Kusini.

Esmael Malude Ramos Nangy anashukiwa kupanga utekaji nyara uliopata dola milioni kadhaa za kikombozi katika miongo miwili iliyopita.

Polisi wa Afrika Kusini walisema alikamatwa katika uvamizi katika nyumba ya kifahari huko Centurion, karibu na mji mkuu wa Pretoria.

Polisi nchini Msumbiji pia walithibitisha kukamatwa kwa mtu anayesakwa mwishoni mwa juma.

Habari za kukamatwa kwa raia huyo wa Msumbiji mwenye umri wa miaka 50 zilitolewa kwa mara ya kwanza na polisi wa kimataifa.

Ilifuatia hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa Julai mwaka jana na mamlaka ya Msumbiji. Taarifa iliyotolewa na polisi wa Afrika Kusini ilisema miongoni mwa vitu vilivyonaswa katika nyumba hiyo ni pamoja na bunduki, katriji, simu tano za mkononi na kadi za benki.

Anafikishwa mahakamani Jumatatu. Msumbiji inataka kurejeshwa kwake. Chanzo cha polisi cha Msumbiji kilisema Bw Nangy alikuwa mshukiwa wa utekaji nyara uliofanyika mwaka jana katika mji mkuu, Maputo.

Utekaji nyara kwa ajili ya fidia ni jambo la kawaida hasa katika miji na miji mikuu ya Msumbiji na walengwa wakuu wamekuwa wafanyabiashara wenye asili ya Asia au jamaa zao.

Kulingana na Huduma ya Kitaifa ya Upelelezi wa Jinai ya Msumbiji (Sernic), nchi hiyo ilirekodi utekaji nyara 13 mwaka 2022 na kukamatwa watu 33 wakihusishwa na uhalifu huo.

Chanzo: BBC Swahil

Post a Comment

Previous Post Next Post