CHUO CHA FURAHIKA KUTOA MAFUNZO YA MALEZI YA WATOTO WADOGO

Na Sophia Kingimali.

Chuo cha Ufundi Furahika kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake katika sekta ya elimu kwa kuanzisha kozi mpya kwa ajili ya kuwasaidia vijana wasiojua kusoma na kuandika,malezi ya watoto wadogo na kozi kwa ajili ya wasaidizi wa ndani ambapo kozi hizo zitatolewa bure kwa watu wa umri kuanzia miaka 5 mpaka 30 lengo kuwasaidia kutimiza malengo yao lakini pia kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Hayo ameyasema leo Januari 5,2024 jijini Dar es salaam Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt. David Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa usaili wa kozi hiyo ambapo usaili huo utafungwa Januari 20,2024.

Amesema mashirika kupitia serikali yameamua kumuunga mkono ili kufadhiri kozi hizo ili watoto wote wa watanzania wasome chuoni hapo bure bila malipo yoyote.

Aidha ametoa wito kwa watu kutokimbilia nchi za nje kufanya kazi kwani nchini kunautulivu na uwekezaji unaongezeka hivyo uwekezaji huo unatoa fursa kwa vijana kujiajiri lakini pia kuajiliwa.

Sambamba na hayo amesema wanatoa elimu bure ya malezi ya watoto kwa wafanyakazi wa ndani na ambao wanaofanya kazi kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo ili kupunguza vitendo vya ukatili vinavyofanywa na walezi kwa watoto wadogo.

Amesema elimu hiyo ya malezi ya watoto inatolewa kwa wale waliomaliza kidato cha nne pasipo kuangalia ufaulu wake.

“Tunawatengenezea huu utaratibu ili wawe na uwezo zaidi wa kuhudumia vizuri watoto hivyo tunawataka vijana wengi wajitokeze kwani sasa hivi kuna shule nyingi za watoto hii itawasaidia kupata ajira”amesema Msuya.

Amesema shule zakulea watoto zinatakiwa kuchukua watu wenye sifa ili waweze kuwahudumia vizuri watoto ili kukomesha ukatili wa watoto unaotokea mara kwa mara.

Akizungumzia kozi kwa walezi wa watoto nyumbani amesema itawasaidia kutimiza malengo yao kwa kasi huku akimlea mtoto kwa upendo na kutimiza wajibu wake wote wa nyumbani.

“Nitoe wito kwa watu wenye hawa wasaidizi nyumbani wawalete ili waweze kupata hii elimu bure kwani itawasaidia katika majukumu yao nyumbani”

Ameongeza kuwa ili kuhakikisha ukatili unaofanywa na hao wasaidizi unakoma kabisa wanatarajia kuwatoa vijana vijijini ambao wanatarajia kufanya kazi hiyo na kuja kuwafundisha ili watakao hitaji wasaidizi hao wawapate hapo chuoni wakiwa tayari na mafunzo ya kile wanachotakiwa kukifanya.

“House Girls wengi wanatolewa vijijini kuna mambo wanayafanya hata wao hawajui kama ni ukatili mwisho wanajikuta kwenye matatizo kwa hiyo ni lazimia tuwafundishe”amesema Msuya.


Post a Comment

Previous Post Next Post