MITAMBO MIWILI YA KUPAKULIA MIZIGO YAPOKELEWA BANDARI YA MTWARA

Katika kutekeleza Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu Bandari ya Mtwara kuwezeshwa kwa vifaa na mitambo ya kisasa ili ifanye kazi ya kuhudumia Shehena kwa ufanisi zaidi, mitambo miwili ya kushusha na kupakia Shehena kwenye Meli ( Mobile Hubour Crane) imewasili na kupokelewa Bandari ya Mtwara.

Akizungumza wakati wa kupokea mitambo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) , Meneja Uhusiano na Mawasiliano Bw. Nicodemus Mushi, amesema kuletwa kwa mitambo hiyo katika Bandari ya Mtwara kutaongeza utendaji kazi katika Bandari hiyo kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari hiyo Bw. Dunstan Kazibure, akiongea kwa niaba ya Meneja wa Bandari ya Mtwara, amesema baada ya kupokea mitambo hiyo iliyotoka Bandari za Tanga na Dar es Salaam, kasi ya kuhudumia Shehena itaongezeka na kufikia malengo kwa haraka na wakati.



Post a Comment

Previous Post Next Post