Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaonya vijana matumizi ya ‘Cha Arusha, Skanka’

MOSHI: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekemea tabia ya vijana kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya hususani bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi kinachojulikana kama Skanka.

Majaliwa ametoa karipio hilo leo Aprili 2, 2024 katika uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru 2024 uliofanyika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema utumaiji wa dawa hizo za kulevya uwafanya kuwa vichaa na kuwapotezea mwelekeo.

“Hivi karibuni kumeibuka aina nyingine ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi inayofahamika kama ‘Cha Arusha’ na ‘Skanka’, aina hii ya bangi yenye sumu nyingi huchanganywa kwenye sigara, lakini ukishaitumia watumiaji wanabadilika na kuwa vichaa,” amesema Majaliwa na kuongeza:

“Huu ni wakati mzuri sasa vijana ambao mmekuwa mkitumia Cha Arusha na Skanka kuacha ili kunusuru maisha yenu, vijana mnahitajika katika Taifa hili, vijana ndio mtakaolijenga Taifa, vijana ndio muelekeo wa Taifa hili, Cha Arusha na Skanka zitawapoteza kwenye mwelekeo na mtalifanya Taifa likose Watanzania,” amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post