MBUNGE MAVUNDE ATIMIZA AHADI YA UJENZI WA UZIO SHULE YA MSINGI UHURU JIJINI,DODOMA.

-Ujenzi wa uzio waanza kwa kasi kubwa

-Wananchi  wapongeza jitihada zake kwenye sekta ya Elimu

-Aishukuru Serikali kwa ukarabati wa madarasa ya shule

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo tarehe 01. 04. 2024 amefanya ziara kukagua ujenzi wa uzio na ukarabati wa madarasa ya Shule ya Msingi Uhuru Jijini Dodoma ambayo ni moja ya shule kongwe za Jijini Dodoma.


Mbunge Mavunde ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa marekebisho makubwa ya miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo kwa shule nyingi za Dodoma Jiji ikiwemo Shule ya Msingi Uhuru.


“Serikali imeleta fedha hapa kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hii kongwe iliyojengwa mwaka 1928,kwa kuwa hali yake haikuwa ya kuridhisha ila kwa ukarabati huu itairudisha shule hii kongwe katika hali yake ya kawaida.


Na mimi kama Mbunge wa eneo hili nimeona niunge mkono jitihada za serikali kwa kuanzisha ujenzi wa uzio wa shule hii kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na kuweka mazingira mazuri ya kusoma kwa wanafunzi ambapo kwasasa eneo hili lina muingiliano mkubwa sana wa wafanyabishara na watoa huduma mbalimbali ambao shughuli zao zinaathiri wanafunzi kusoma kwa utulivu”Alisema MavundeAkitoa shukrani kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Uhuru Mh. Khalfan Kabwe ameshukuru na kupongeza jitihada za serikali za ukarabati wa madarasi na ujenzi wa uzio unaofanywa na Mbunge wa Dodoma Mjini na kuahidi kusimamia utekelezaji wa miradi hii kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post