HATUTAMWACHA YEYOTE ANAYEIBA FEDHA ZA UMMA – KWAGILWA

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Reuben Kwagilwa, amesema hawatamuacha mtu yeyote anayehusika na wizi au ubadhirifu wa fedha za umma, akisisitiza kuwa watumishi wote wazembe na wanaodokoa fedha watawajibishwa.

Kwagilwa ameyasema hayo leo, Desemba 17, 2025, katika Mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe, wakati akizungumza katika ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, mkoani humo.


Amesema yeye pamoja na timu yake watafika katika mikoa yote 26, Halmashauri zote 184, pamoja na wilaya, kata na tarafa zote, kuwabaini na kuwachukulia hatua watumishi wazembe, wabadhirifu na wanaoiba fedha za umma.


“Hatutabaki kwenye Halmashauri peke yake. Tutashuka hadi wilaya, kata na tarafa zote. Hatutamuacha mtu yeyote anayedokoa fedha za umma,” amesema Kwagilwa.


Ameongeza kuwa ukaguzi na ufuatiliaji utafanyika hadi vitongoji na vijiji vyote nchini, akisisitiza kuwa yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha alizokabidhiwa atawajibishwa



Post a Comment

Previous Post Next Post