Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi OWM–TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, Mhe. Kwagilwa ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua kituo hicho ambacho ujenzi wake uligharimu zaidi ya Shilingi bilioni 54.5, lakini hakijatimiza matarajio ya serikali na wananchi, huku idadi ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi yanayotumia kituo hicho ikiwa bado ni ndogo.
“Timu hiyo itusaidie kufanya tathmini ya mradi huu kulingana na malengo yake ya awali, ufanisi wake, miundombinu iliyopo, huduma zinazotolewa, pamoja na mapato yanayopatikana au kupotea tangu kituo hiki kikabidhiwe kutoka Jiji la Dar es Salaam kwenda Halmashauri ya Ubungo,” amesema Mhe. Kwagilwa.
Amesisitiza kuwa ndani ya siku 90, timu hiyo inapaswa kuwasilisha ripoti kamili yenye mapendekezo ya namna ya kuboresha uendeshaji wa kituo hicho ili kiweze kutoa huduma bora kwa wananchi na kuongeza mapato ya serikali.
Timu hiyo itajumuisha wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na itahakikisha changamoto zote zinazoathiri matumizi kamili ya kituo hicho zinabainishwa na kupatiwa suluhisho.


Post a Comment