Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe mwenye shati la Kitenge wa pili kushoto akitoa maagizo kwa msisitizo huku akionesha ishara ya mikono kwa Mamlaka ya Maji Mjini kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi chanzo cha maji cha Mto Ikolongo wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Mjini Mpanda Mama Anna Lupembe Mwenye Tishirt nyeupe pamoja na viongozi wengine wa Halmashauri ya Mji Mpanda.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na taka wa Mji wa Mpanda Mhandisi Zacharia Nyanda mwenye shati nyeupe na anayenyosha mkono kuonesha eneo la chanzo wakati akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi wa Katavi Dkt Rutengwe anayemsikiliza kwa umakini kuhusu chanzo cha maji cha Mto Ikolongo akimweleza kuwa eneo hilo ndio mradi wa Maji ya Mseleleko yanayotumiwa na wakazi wa Mjini.
Wakazi wa Ikolongo makazi ya Wakimbizi Katumba wakitoka kuchota maji kwenye chanzo cha maji ya mto huo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu.
…………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu-Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe, ameiagiza Mamlaka ya Maji mjini Mpanda kwa kushirikiana na Idara ya Maji pamoja na Idara ya Mazingira kulinda na kuhifadhi chanzo cha maji cha mto Ikolongo ambacho ni tengemeo kubwa kwa Mseleleko yanayotumiwa na Wakazi wa Mji wa Mpanda.
Dkt Rutengwe alitoa agizo hilo muda mfupi baada ya kutembelea chanzo hicho na kujionea hali halisi katika mto huo ulioko umbali wa takribaini kilometa 24 kutoka Mjini Mpanda.
Mbali ya kuhifadhiwa pia ameagiza kupanda miti kuzunguuka chanzo hicho kilichopo eneo la Ikolongo Makazi ya Wakimbizi Katumba.
Pamoja na kuhimiza kulinda chanzo hicho pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Maji safi na taka katika Mji wa Mpanda kwa kushirikiana na Uongozi wa Halmashauri kuona namna ya kuwatengenezea miundombinu ya maji wakazi wanaoishi jirani na chanzo vyanzo vya maji ili waweze kuwa na moyo wa kuvilinda.
Iwapo watapatiwa huduma ya maji itakuwa rahisi kwao kwa kuwa na moyo na ari ya kuendelea kulinda na wala hawawezi kuharibu mazingira ya vyanzo vya maji kwa kuwa wanafahamu umuhimu na manufaa yake kwao.
Iwapo watatengenezewa mabomba na kuwekewa maji ya bomba yanayotoka katika chanzo wanachohifadhi watakuwa waelewa na watanufaika na wenyewe kuliko kuwaacha kama walivyo
Akaongeza kuwa iwapo watatumia maji ya kwenye chanzo inachangia kwa njia moja au nyingine kuharibu mazingira pamoja na uchafuzi zaidi kwa kuwa maji hayo yanatengemewa na watu wengi kwa maisha yao.
“Hakikisheni wananchi hao wanaoishi jirani na chanzo hiki wanapata maji ili wasiendelee kuharibu chanzo hiki wasiendelee kufulia na kunyweshea mifugo yao katika chanzo hiki kilindwe na kutunzwa,iwapo mtafanya hivyo mtakuwa mmesaidia sana kuoko chanzo hiki.”alisema Dkt Rutengwe.
Akiongelea namna ya kuweza kupaendeleza na kupahifadhi ili kuweze kuwapa umuhimu zaidi,ameeleza kuwa chanzo hiki ni utajiri mkubwa na huenda ikawa Mkoa wa kwanza wenye chanzo cha maji kizuri kilichohifadhi na kutunzwa vizuri hivyo haina budi kuendelea kukilinda na kukihifadhi kwa gharama yeyote huu ni utajiri wa kipekee,huwezi kuwa masikini ukiwa na chanzo kizuri namna hiyo alieleza Mkuu wa Mkoa huyo.
Akizungumzia kuwazuia wananchi kutumia eneo hilo kwa shughuli za kibinadamu kama kuchota maji,kufua na shughuli nyingine alieleza kuwa huwezi kumzuia mwananchi akakuelewa bila kuweka utaratibu mzuri wa namna atakavyoweza kuendelea kupata huduma aliyokuwa akiipata.
“Haiwezekani kumkataza mwananchi kuchota maji katika eneo hili wakati hujamwandalia mazingira mazuri mbadala ya yeye kupata huduma ya maji,hilo halikubaliki watengenezeeni haraka sana mazingira ya wao kupata huduma ya maji kisha ndio muweke utaratibu mzuri wa kuwakataza wasitumie kuja kuchota maji, wala kutumia eneo hili kwa shughuli za kibinadamu kwa kuwa shughuli za kibinadamu zitaharibu chanzo hiki”alisema Mkuu wa Mkoa kwa Msisitizo.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Anna Lupembe alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa eneo hili ni hazina kwao na wameweka mpango mzuri wa kuliombea fedha kutoka wizarani ili kuliendeleza na kuwapatia maji safi wananchi wa Mpanda na Mkoa kwa ujumla.
Mwenyekiti huyo alieleza kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mhandisi Zacharia Nyanda alipofika tu katika Mkoa huo Halmashauri ya Mji wa Mpanda alitengeneza maandiko ya kuomba fedha kwa ajili ya kuweza kuendeleza chanzo hiki ili kiweze kuwanufaisha wananchi wa Mpanda waweze kupata maji safi.
Alisema kutokana na Andiko lililoandikwa kuomba fedha zimepatikana karibu shilingi bilioni tatu ambazo ziatasaidia kusambaza maji katika mji wote wa mpanda na maeneo ya jirani kwenye vijiji vinavyozunguuka Mji huo, ameyataja maeneo yaliyoko nje ya mji ambayo yanaweza kunufaika na mradi huu wa maji kutoka chanzo cha maji mto Ikolongo kuwa Vijiji vilivyoko Kata ya Magamba Halmashauri ya Nsimbo,Mtapenda,Kasokola Nsimbo yenyewe, Milala,na Kakese.
Post a Comment