Chama tawala CCM kimesema kuwa kitafanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua dhidi ya Waziri mkuu wa nchi hiyo Mizengo Pinda iwapo matamshi yake ya kutangaza nia ya kuwania Urais wa nchi kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani uliambatana na vitendo vya kufanya Kampeini.
Awali chama hicho kiliwahi kuwaonya baadhi ya vigogo kadhaa ambao walionyesha kuanza kufanya kampeini mapema ambapo sasa kufuatia hatua ya Kigogo huyo ambaye ni Waziri mkuu aliyeko madarakani inaanza kufungua mwanya katika mbio za kuelekea Ikulu hapo mwakani.
Erick David Nampesya amezungumza na Katibu wa Itikadi wa CCM Nape Nnauye ameanza kwa kusema kutangaza nia ya kuwania Urais siyo kosa kisheria.
Nape alipoulizwa na mwandishi wa BBC Swahil kuwa hatua ya Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda kujitokeza mbele ya hadhara akiwa Mwanza akitamka wazi kuwa atagombea Urais ni kama vile ameshapuliza kipenga cha kuelekea Magogoni? (Ikulu)
Nape alijibu na nukuu "yeye sio mwenye mamlaka yakupuliza kipenga na kanuni za chama na taratibu zipo juu ya kila mtu, na hizi kanuni zipo juu hata ya Mwenyekiti wa chama, wote tunapaswa kuzifuata hazitojali cheo cha mtu, hizi kanuni zimetengenezwa siku nyingi kabla ya mimi sijazaliwa (Nape) na zimekuwa zikitumika na Mwalimu alikuwa akiziheshimu Mwalimu ambae ni Muasisi wa Chama hiki. Kama (Pinda) atakuwa amevunja kanuni na taratibu, kanuni hizi azihathiriwi na cheo cha mtu".
Mbona unasita kusema kama kweli amevunja kanuni za chama?
"Nasitakusema kwasababu mimi sio mamlaka ya kusema kama ndio amevunja, hata wale walioadhibiwa sikusema mimi vilisema vikao, hailuwa Katibu mkuu, haikuwa Naibu Katibu mkuu, hakuwa Mwenyekiti wala haikuwa Makamu Mwenyekiti, n.k bali vilikuwa vikao na vilifanyika baada ya uchunguzi, hata hili lililotokea juzi ni lazima lichunguzwe, kama ni kweli alikutana na watu na walifanya nini na hao watu walipokutana; vikao vikijiridhisha ripoti hiyo ikaletwa ndani ya vikao ndio itazungumzwa halafu sasa watasema amekosea au hakukosea". Alijibu Nape.
Swali. Hamuoni kama halii kama livyofanya Bw. Mizengo Pinda italeta mpasuko ndani ya chama ukizingatia ni mwaka mmoja ulibaki kwa ajili ya uchaguzi wa Rais?
"Mpasuko unaletwa na matendo ambayo ni kama nilivyosema ni yakuanza kutafuta wafuasi, lakini ukisema utagombea halafu ukakaa kimya hili kwetu halijawahi kuwa na mpasuko, na ninasemaa hii sio mara ya kwanza, mwaka 1995 tulikuwa na wagombea 11 na wote walitangaza nia na halikuwa tatizo ila tatizo linakuja pale utakapo tangaza ni matendo gani utayafanya baada au kabala ya kutangaza, ikiwa umeanza kutafuta wafuasi hilo ndio linakuwa ni tatizo" .Alijibu Nape.
Post a Comment