Meneja
wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza
Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa
redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea
uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na
shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Sengerema
OFISI
ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha
Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama
vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili
kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa
kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani
(DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice
Stephano wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao
ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Sengerema.
Beatrice
alikuwa akizungumzia mradi anaousimamia ambao umedhaminiwa na UNDP
kupitia UNESCO kwa ajili ya kuelimisha umma wa watanzania kupitia redio
za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi 2015.
Alisema
uamuzi wa kutumia redio za jamii unatokana na redio hizo kuwafikia
wananchi wengi zaidi, hali ambayo wadau katika masuala ya demokrasia
wameona kwamba inaweza kutumika kuboresha zaidi uelewa wananchi.
Mratibu
wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano (wa pili
kushoto) akizungumza na mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria
warsha ya siku tano inayofanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano
cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza kuhusiana na ofisi yake kufanya
kazi kwa pamoja na redio za jamii nchini katika kutoa elimu kwa umma.
Naye
Afisa mfawidhi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani
Mwanza, Ludovick Ringia akizungumzia sheria mbili za vyama vya siasa
alisema kwamba ni wajibu wao kuwaeleza wananchi kuhusu maadili na kanuni
katika sheria zinazogusa ukuzaji wa amani katika duru za siasa na
demokrasia.
Alisema
mradi huo wa kuelimisha wananchi ambao unafanyika kwa udhamini wa
Unesco kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) ni moja ya njia za kufanikisha amani katika kipindi chote kuanzia
uchaguzi wa mwisho hadi mwingine.
Alisema wanatumia redio za jamii kwa kuwa redio za kibiashara zimekuwa kikwazo hasa bajeti inapouma kidogo.
Alisema
mradi huo ambao unafanyika kwa mwaka mmoja ni sehemu ya juhudi za
taasisi hiyo za kuliwezesha taifa kuendelea kuwa na utulivu.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
(wa pili kulia), akielezea uwezo wa redio za jamii zinavyoweza kufikia
jamii kubwa zaidi nchini wakati ujumbe kutoka ofisi ya msajili wa vyama
vya siasa ulipofanya mazungumzo na Wenyeviti wa Bodi na Mameneja wa
redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyofadhiliwa
na shirika maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO
iliyofanyika kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema
mkoani Mwanza.
Wenyeviti
wa bodi na mameneja hao katika warsha hiyo walielemishwa uboreshaji wa
masoko na umuhimu wa redio za jamii juu ya matumizi ya Tehama kwa ajili
ya kuongeza ufanisi wa kazi na kushirikisha zaidi wananchi.
Aidha
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Al Amin Yusuph
akizungumzia mafunzo hayo alisema kwamba mradi huo umekuja wakati
muafaka ili kutoa elimu kwa umma, kwani kutokana na tafiti mbalimbali
zilizofanywa takribani asilimia 70 ya wananchi wanaoishi vijijini
wanasikiliza redio huku asilimia 5 tu ndio wanaangalia runinga.
Meza
kuu: Kutoka kushoto ni Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama
vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko, Mratibu wa
Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa
vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Mwenyekiti wa Warsha
hiyo kutoka Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara, Bw.Baraka Ole
Maika (katikati), Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mfawidhi
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick
Ringia (kulia).
Uelewa
huo upo katika sheria za uchaguzi, gharama na kuona wajibu wao wa
kumsaidia Msajili wa Vyama vya Siasa kukabiliana na mazingira hatarishi
ya amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Alisema
ni kazi ya Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria ya vyama
namba tano ya mwaka 1992 ya kusajili vyama na kuviangalia na ile ya
namba sita ya mnwaka 2010 ambayo inagusia gharama za uchaguzi.
Mratibu
huiyo amesema kwamba timu kutoka Ofisi ya Msajili itafika kwenye redio
hizo za jamii na kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali
yanayohusu mustakabali wao katika siasa na kuimariuka kwa demokrasia.
Aidha
elimu hiyo inatarajiwa kuwasaidia wananchi kutambua kwamba wana wajibu
katika kuhakikisha kwamba menejimenti za uchaguzi zinawajibika pamoja na
muuingiliano wake ili kuwa na michakato salama ya cuhaguzi na uchaguzi
wenyewe.
Afisa
Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw.
Ludovick Ringia (kulia) akielezea ufanyaji kazi wa sheria mbili za vyama
vya siasa kwa wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini
wakati wa warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na SIDA na kuratibu na
UNESCO ambayo imefanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
Afisa
Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani
Mwanza, Bw. Isaya Makoko akiwasilimia wenyeviti wa bodi na mameneja wa
redio za jamii nchini (hawapo pichani).
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akihoji swali kwa ujumbe uliotoka kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za
jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyomalizika mwishoni
mwa juma kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza kwa ufadhili wa
SIDA na uratibu wa UNESCO.
Post a Comment