TAMASHA LA WANAFAMILIA LA AIRTEL LAFANA FUN CITY WEEKEND

Wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Kema Mabango, Abdallah Gunda na Jackson Mmbando wakishiriki katika shindano la kukuna nazi wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
Washindi wa shindano la kukuna nazi wakishow love. Kutoka
(kushoto), Mshindi wa Kwanza, Abdallah Gunda, Mshindi wa Pili, Jackson
Mmbando na Mshindi wa Tatu, Kema Mabango.
Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakiogelea wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakishiriki katika michezo  wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
 Wafanyakazi wa Airtel na familia zao wakijisevia maakuli.
    Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akiwahudumia chakula wafanyakazi wa Airtel na familia zao.
 
Na Mwandishi wetu.
 
•       Airtel Family day yalenga kuongeza hamasa kwa wafanyakazi kujituma
katika kazi zao
Imeelezwa kuwa ufanisi wa watumishi katika ngazi mbali mbali za
kiutendaji unaweza ukaongezeka pindi wafanyakazi wanapokutana pamoja
na kubadilishana mawazo na viongozi wao katika hali ya kiurafiki.

Akizungumza katika tamasha la siku ya familia ya kampuni ya simu za
mkononi ya airtel, Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo SOPHIA
MELAMALI, amesema kuwaweka wafanyakazi katika eneo moja na familia zao kunadumisha mshikamano baina ya wafanyakazi  na familia zao kitendo
kinachoongeza ufanisi katika eneo la kazi.

“Airtel tumejipanga kuwa na muundo mzuri wa kufurahia matunda ya kazi
yetu na falilia yetu kwa kuwa hii inasaidia sana kuwafanya wafanyakazi
wetu kukutana, kufahamiana na kufurahi na familia zao  na hatimae
kupunguza msongo wa mawazo ya kawaida ili kuendelea kufanya kazi ya
kuhudumia wateja wetu vyema” alisema SOPHIA MELAMALI Meneja Rasilimali Watu Airtel.

Nao baadhi ya wafanyakazi wa airtel wamepongeza kitendo cha kampuni
hiyo kuandaa tamasha hilo na kubainisha kwamba ni sehemu ya
kuwawezesha wafanyakazi kufahamiana.

Wamesema tukio hilo linawawezesha wafanyakazi kupumzika na familia zao
pamoja na wafanyakazi wenzao katika mazingira tulivu na a kirafiki
ADRIANA LIAMBA Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Airtel sisi wafanyakazi wa Airtel  tumefarijika sana na jinsi ambavyo leo uongozi na kampuni  yetu ilivyotukutanisha na familia zetu zote ili tuweze kufurahia,  hii
pia inatupa moyo wakuendelea kuwahudumia wateja ipaswavyo na pia
kushiki katika mambo ya kijamii zaidi kwa kuziona fulsa zilizomo leo
na baadae”

“Mfano familia zetu tumekutana watu wa aina tofauti zikiwa na
wafanyakazi wa baadhi ya mashirika mengine nchini, hii pia ni fulsa
kwetu kuendelea kutengeneza wateja tutakaowahudumia kwa sasa au
kuwekeza kwa watoto wetu ili waje kuwa wateja wa baadae,  kwa kweli
family day party ni nzuri” alimaliza kwa kusema Bi Lyamba.

Baadhi ya watoto walioshiriki katika tamasha hilo ANTHONY NABOLI na
FRANCIS ALEXANDER hawakusita kuonyesha hisia zao baada ya kucheza
michezo ya aina mbali mbali kwa kuwashuru sana wazazi wao kwa
kuwawezesha wao kushiriki michezo mingi katika viwanja vya FUN CITY
pamoja na kupewa zawadi nyingi.

Nae afisa rasilimali watu wa Airtel na mratibu wa Family party hiyo
Bw, Mubaraka Kibarabara alisema “tamasha letu la familia mwaka huu
limekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa kuwapa nafasi wafanyakazi siku
nzima wakicheza michezo mbalimbali na kufurahi ikiwemo ile ya kuvuta
Kamba, kuimba karioke, kuogelea, kubembea katika mashine za kisasa, na
kuwepo kwa shindano la kipekee kabisa lililovuta hisia za wengi la
wanaume kushindana kukuna nazi.

Post a Comment

Previous Post Next Post