Guy Scott
ambaye alikuwa makamu wa rais Zambia wakati wa utawala wa Michael Sata
ametajwa kushika nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa sasa mpaka pale ambapo
ataapishwa mara baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.Waziri
wa ulinzi Zambia Edgar Lungu amesema maandalizi ya uchaguzi huo
yataanza muda wowote ambapo katiba ya nchi hiyo inaagiza kufanyika
uchaguzi wa Rais ndani ya siku 90 baada ya kufariki kwa aliyekuwa rais
wa nchi hiyo.
Scott
ameteuliwa kushika wadhifa huo ambapo hii itakuwa mara ya kwanza kwa
rais mzungu kuongoza nchi ya Afrika tangu kuisha kwa kipindi cha ubaguzi
wa rangi Afrika Kusini chini ya utawala wa FW de Klerk.
Kulikuwa
na utata uliotokana na katiba ya Zambia kumruhusu Scott kushika wadhifa
huo kwa sababu wazazi wake wanatokea Scottland, huku katiba hiyo ikitaja
rais wa nchi hiyo ni lazima awe Mzambia kamili kwa maana ya kwamba
wazazi wake wote wawili wanapaswa kuwa wamezaliwa nchini humo.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI ZAMBIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.
Post a Comment