Mkurugenzi mkuu wa hospital ya
Kairuki, Dkt Asser Mchomvu (kulia) akiwa amebeba tuzo aliyokabidhiwa na
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal (kushoto). Picha na mpigapicha wetu.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ameukabidhi uongozi wa
Hospitali ya Kairuki (KH) tuzo ya waliofanya vizuri katika vigezo
mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya katika mkutano wa 4
wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya uliofanyika
wiki iliyopita (Octoba 31-2014) katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu
ya Tanzania jijini Dar es salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Naibu MKurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Muganyizi Kairuki alisema
sifa ya mafanikio yao mpaka wakapata tuzo hiyo yanatokana na mafunzo kwa
wafanyakazi wa Hospital wapatao 20 yaliyoendeshwa na Wizara ya afya
ikishirikiana na Jhpiego,CDC na PEPFAR.
Dkt. Kairuki aliongeza kuwa ni
mafunzo kuendelea kutolewa na wakufunzi wa ndani ( inhouse training),
kuundwa kwa timu maalum ya ndani kwa ajili kufanya ukaguzi wa kushtukiza
ndani na utayari wa KH kushirikia katika zoezi la udhibiti na uzuiaji
wa maambukizi.
Aidha, Dkt. Kairuki alieleza kuwa
siri nyingine ni ushirikiano mzuri baina ya manegimenti ya KH na timu ya
wakaguzi toka wizara ya Afya katika kutekeleza maagizo na mapendekezo
na kuyafanyia kazi.
“Kwa upande wetu maeneo
yaliyofanya vizuri katika zoezi ili ni pamoja na mashine bora za kuuwa
vijidudu (sterilization unit) na eneo zima katika kitengo hicho, eneo la
kuifadhi/ kutenganisha na usafirishaji wa taka hatarishi, taka mbichi
na taka mchanganyiko pia chumba cha upasuaji kufuata taratibu stahiki za
kimataifa katika kuzithibiti maambukizi,” alisema Dk Kairuki
Aliongeza kuwa wakati huohuo KH
imezindua kampeni maalum za muda mrefu katika kuchunguza na kutibu
magonjwa yasiyoambukiza, mfano saratani ya matiti, saratani ya shingo ya
kizazi na saratani ya tezi dume (prostate).
Saratani hizi ndizo zinazoongoza kwa hapa nchini.
“Lakini pia KH imezidi kuboresha
huduma katika vitengo vya macho, sikio, pua na koo kwa kupata mitambo ya
kisasa katika nyanja hizo,” alisema Dk Kairuki
Aliongeza kwakusema kuwa KH
imezindua wodi mpya ya kisasa hasa kwajili ya wanachama wa mfuko wa Bima
ya taifa ya afya.(NHIF) na wodi maalum ya watoto.
Wengine waliotunukiwa tuzo hizo za
uboreshaji wa huduma za afya ni Hospitali ya Bugando-Mwanza pamoja na
Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC).
Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).
Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).
Post a Comment