Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania
imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda
Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya
Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili.
Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria
wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema
baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh
Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali
ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine
ya madai ya uchochezi, Mkoani Morogoro inayomkabili.
(PICHA/HABARI : DEOGRATIUS MONGELA/GPL)
Wakili wa Sheikh Ponda, Bw Juma Nassoro akizungumza jambo na mteja wake mahakamani hapo.
Sheikh Ponda akitoka nje ya Mahakama Kuu baada ya kushinda
Kesi ya Ardhi iliyokuwa ikimkabili kisha kurudi mahabusu katika gereza
la Segerea.
Post a Comment