LADY JAYDEE:  KAMWE SITARAJII KUFANYA SIASA MIMI NI MUZIKI TU

 Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee'
 Lady Jaydee akisoma gazeti la Staa Spoti.
 Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Jambo Leo, Frank Balile (kulia), akimuelekeza jambo Lady Jaydee wakati akimuonesha gazeti hilo.
Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, alipotembelea chumba cha habari Dar es Salaam jana.

Dotto Mwaibale

MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' amesema kamwe atarajii kujiingiza katika masula ya siasa kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo Dar es Salaam jana, baada ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti hilo katika Jengo la Hifadhi House katika makutano ya Barabara za Azikiwe na Samora.

"Binafsi sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao.

Alisema anafurahi kufanya mziki na wala hajuti kwa kuwa unamuongezea kipato kikubwa ni kutunga nyimbo zenye mahudhui na mvuto na kwa wakati husika.

Baadhi ya wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule 'Profesa J, Khadija Shabani 'Keisha' Ummy Wenslaus 'Dokii, na wengine kama Fullgence 'Mwanacotide' ambaye yupo Chadema.

Post a Comment

Previous Post Next Post