MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RUNGU KICHWANI WILAYA YA CHUNYA.
MTU MMOJA GASPER VISENTI [38],
MKAZI WA KIJIJI CHA KALANGALI ALIKUTWA AMEUAWA PORINI BAADA YA KUPIGWA
RUNGU KICHWANI NA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MOJA LA CLEMENT
SIMKOKO @ YOHANA, MKAZI WA [W] MBOZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
12.11.2014 MAJIRA YA SAA 16:15HRS KATIKA KITONGOJI CHA IVUMWE, KIJIJI
CHA KALANGALI, KATA YA MTANILA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKITOKA DAMU NYINGI PUANI NA MASIKIONI.
CHANZO CHA TUKIO HILI NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MAREHEMU KUMDHURUMU
MTUHUMIWA PESA UJIRA WAKE BAADA YA KUMLIMIA SHAMBA LA TUMBAKU. HATA
HIVYO MTUHUMIWA HUYO ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI AN AENDELEA
KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA PIA KUEPUKA MATATIZO YANAYOEPUKIKA. AIDHA ANATOA
WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE
ZIWEZE KUCHUKULIWA MARA MOJA.
TUKIO LA PILI.
MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA KUGONGWA NA PIKIPIKI WILAYA YA KYELA.
MTOTO MMOJA AITWAE MICHAEL MICHAEL
[4], MKAZI WA NDANDALO ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
PIKIPIKI T.207 CUV AINA YA SUNLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MOSE ANDREW
[22],MKAZI WA NDANDALO.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS
KATIKA KIJIJI CHA NDANDALO, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA
YA KYELA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA,
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
TUKIO LA TATU.
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WILAYA YA ILEJE.
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WANAOSOMA SHULE YA MSINGI ILOMBA AMBAO NI 1. SEVELINA MWILE [11], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE 2. GRACE PATSON [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE NA 3. AGEY SEME [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ILOMBA[W] MBEYA VIJIJINI WOTE WANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULENI HAPO WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WAKATI WAKICHIMBA UDONGO NDANI YA SHIMO.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
12.11.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ILOMBA, KATA
YA ITALE,TARAFA YA BUNDALI WILAYA YA ILEJE MPAKANI NA WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI,MKOA WA MBEYA. AWALI KABLA YA KUKUTWA NA MAUTI WAHANGA HAO
WALICHUKULIWA SHULENI NA ISAMBI MWASENGA [57], MWALIMU MKUU MSAIDIZI WA
S/MSINGI ILOMBA KWENDA KUMFANYIA KAZI BINAFSI YA KUCHIMBA UDONGO NA
KUMPELEKEA NYUMBANI KWAKE. MIILI YA MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI WA
KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA YUPO
MAHABUSU KWA AJILI YA USALAMA WAKE WAKATI UPELELEZI WA SHAURI HILI
UKIENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUWATUMIKISHA KAZI WATOTO WENYE UMRI MDOGO KATIKA
MAENEO/MAZINGIRA HATARISHI YATAKAYOWEZA KUSABABISHA MAAFA NA KUFANYA
VITENDO VYA NAMNA HIYO NI KWENDA KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa;
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment