Na Kibada Kibada –Arusha
WAHADZABE
Imeelezwa kuwa mjibu wa tafiti
mbalimbali zilizofanyika hapa nchini kwa mwaka 2010 yanaonesha kuwa
Jamii ya kabila la wahadzabe 1,300 hapa nchini wanaishi katika wilaya
ya Mkalama Mkoani Singida hivyo iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa
kuyalinda makabila hayo madogo huwenda yakatoweka.
Akiwasilisha mada inayohusu
tathimini ya mchango wa ufugaji nyuki kwa maisha bora kwa wahadzabe
Mkoani Singida,kwenye Kongamano la ufugaji nyuki Afrika linalofanyika
kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha.
Mtafiti na Mtaalamu wa familia
kutoka chuo kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Philimon Kiemi ameeleza kuwa
kwa mjibu wa utafiti uliofanyika Mkoani Singida kwenye Wilaya ya
Mkalama inaonesha Jamii ya kabila la Wahadzabe wapo 1,300 na kati yao
356 wanaishi katika wilaya ya Mkalama Kijiji cha Maguli wapo katika kaya
zipatazo 70.
Kiemi anaeleza kuwa katika
utafiti wao kaya 30 zilizofanyiwa utafiti walibaini kuwa wahadzabe
wanaishi kwa kutengemea mimea,mizizi,matunda,kula ndege na wanyama
wanaishi kukusanya matunda,kula ndege,na wanyama na mizizi ili waweze
kuishi.
Anaeleza kuwa wahadzabe
wanaamini kuwa asali ni dhahabu kwao kwa kuwa ni chakula na dawa
kwao,kuhusu ufugaji wa nyuki wao ili kupata asali wanatumia mbinu ya
kutoboa miti aina ya mibuyu kisha kuiziba na kuacha tundu na nyuki
huingia na kutengeneza asali ambayo huitumia kama chakula.
Wahadzabe wao wana nyuki aina
sita kwa mjibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2013 uliofanywa na David kwa
mjibu wa utafiti huo pia ulibaini wahadzabe 56.7 hawajui kusoma
asilimia 15 walisoma elimu japo ya sekondari,msingi na asilimia 3
hawajasoma na kunaidadi kubwa ya watoto ambao hawasomi katika jamii ya
wahadzabe.
Jamii ya wahadzabe wenye umri wa
kuanzia mika 30-60 wanauzoefu katika ufugaji nyuki na kati yao asilimia
63 walisema kuwa nyuki zinaongeza uchumi katika eneo lao.
Pia jamiii ya wahadzabe walio
wengi hawajui Kiswahili,na wakaeleza kuwa asilimia 77 wanasema
wanalisema nyuki ni muhimu kwao, na asilimia 63 wananufaika na nyuki,kwa
wastani wote walikubalikuwa ufugaji nyuki ni muhimu kwa maendeleo yao.
Hata hivyo asilimia 50
wanakabiliwa nahuduma duni ya miundombinu wakaeleza kuwa ufugaji nyuki
utawasaidia kuinua uchumi na kipato chao.
Wakizungumzia asali walisema
wanatumia asali kama chakula ambapo kati yao asilimia 83.5 walieleza
kuwa kuwa asali inatumika kama chakula kwao na jamii hiyo haina uzazi
unaongezeka kama jamii nyingine.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Pascal Kone alieleza kuwa katika kutambua na kujali jamii hiyo
serikali imepima eneo lao na kulipatia hati ambapo almwagiza mkuu wa
wilaya ya Mkalama kuhakikisha anawaondoa wavamizi wote waliovamia eneo
la wahadzabe wanaondoka mara maja na ifika mwezi desemba kama watakuwa
hawajaondoka atawondoa kwa nguvu.
Mkuu huyo wa Mkoa alieleza
kuwajuhudi nyingine zilizofanyika ni kuwachimbia visima vya maji ili
wawe na maji yatakayowatosha wao kwani iwapo watawawekea maji mengi
zaidi wanaweza kuvamiwa na wafugaji .
Mbali ya kuchimbiwa visima pia
wamejengewa shule,na zahanati, nyumba za waganga shule ya maguli pia
imejengwa na mabweni mawili ya wavulana na wasichana ili waweze kusoma.
Ambapo ifikapo mwakani mwezi
januari watoto wapatao 40 wa kihadzabe wataanza kusoma katika shule hiyo
iliyojengwa lengo ikiwa ni kuwapatia elimu ili nao waweze kuijua dunia.
Wahadzabe hao walipelekewa
majembe ili waanze kujifunza kilimo lakini wameyatumia na kuyabadilisha
kuwa visu,pia wamepewa mizinga 150 ambayo wanaitumia kwa kufugia nyuki.
Kwa upande wao kiongozi wa
kabila la Wahadzabe aliyefahamika kwa jina moja la Jacob aliiomba
serikali kuona utaratibu wa jinsi ya kuwazuia wavamizi wa maeneo yao
wanaowavaimia katika makazi yao ya asili waliyowazoea.
Akasema kama wanaingia kwenye
eneo lao wafuate utaratibu na wao wana haki ya kuishi kadri mungu
alivyowajalia,wakaeleza kuwa kwa kuwa wao walikuwa hawajui kutumia ardhi
sasa wamekuja watu wanaojua kuitumia lakini wanaojua matumizi ya ardhi
lakini wafuate utaratibu.
Mzee Jacob akaeleza kuwa iwapo
watavamiwa ardhi yao watakwisha kwa kuwa wanaishi kwa kutegemea
mistu,kwa kukusanya matunda, mizizi kuwinda wanyama na ndege ambacho
ndiyo chakula chao kikuu.kwani wakiwa na mistu wanapata nafasi ya
kukusanya matunda na vyakula vingine wanavyotegemea kutoka mstuni hivyo
wanachoomba serikali iwasaidie kuwalindia eneo lao kwa kuwa nao ni
watanzania kama wengine.
Aidha itaendelea kuwalinda
kuwasaidia wahadzabe wandorobo na wasandawe ambao makabila madogo
amabao wapo porini hapa nchini na wako katika hatari ya kutoweka
katika ramani ya Tanzania kwa kuwa nao ni watanzania kama walivyo
watanzani wengine.
Post a Comment