ACACIA YATUMIA MILIONI 400 KUJENGA MAABARA SHINYANGA

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Mhandisi Philbert Rweyemamu(kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro wakati wa uzinduzuzi wa jengo la Maabara katika shule ya Sekondari Ngokolo lililojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Buzwagi.
Jengo la Maabara lililojengwa kwa ufadhili wa Mgodi wa Kuchimba Dhahabu wa Buzwagi katika shule ya sekondari Ngokolo iliyopo wilani Shinyanga.
Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari Ngokolo iliyopo wilayani Shinyanga wakishuhudia uzinduzi rasmi wa vyumba vya Maabara uliojengwa kwa ufadhili wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Maabara itakayotumik kwa ajili ya kujifunzia masomo ya Sayansi.
Add caption
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Mhandisi Philbert Rweyemamu akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kukabidhi majengo ya Maabara hizo.
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya Maabara hizo.
Mkuu wa wilaya Shinyanga Bi Josephine Matiro akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia kukabidhiwa kwa maabara hizo ambazo zimejengwa kwa msaada wa Kampuni ya Kuchimba Dhahabu ya Acacia kupitia Mgodi wa Buzwagi.
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mh. Steven Masele akitoa maneno ya shukurani kwa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia kwa msaada wa ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule za sekondari katika manispaa ya Shinyanga
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama na kamati za shule zilizonufaika na msaada huo wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi wa wilaya.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakizungumza na mbunge wa Shinyanga mjini juu ya utekelezwaji wa agizo la Rais Dr Jakaya Kikwete la kuhakikisha kila shule inakuwa na maabara ya sayansi.
Afisa miradi ya maendeleo ya jamii wa mgodi wa Buzwagi Moses Msofe akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais wakati walipokuwa wakikagua miradi hiyo kabla ya kukabidhiwa rasmi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Philbert Rweyemamu akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro jengo la maabara la shule ya Sekondari ya Mazinge ambalo limejengwa kwa ufadhili wa kampuni yaKuchimbaDhahabu ya Acacia. Anayepiga makofi ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mh Steven Masele.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.

Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Acacia kupitia mgodi wake wa Buzwagi imetumia zaidi ya shilingi Mil 400 kukamilisha miradi minne ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika Shule za sekondari za Mazinge, Kizumbi, Ngokolo na Old Shinyanga zote za Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi maabara hizo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Philbert Rweyemamu amesema, Acacia imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yote ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya kampuni ya kufanya uchimbaji unaojali na hususani kwa kutekeleza miradi katika maeneo yanayozunguka migodi ya Acacia.
Kukamilika kwa miradi hii kunatajwa kuwa kutasaidia katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wa sayansi katika maeneo mbalimbali hapa nchini “Matumaini ya Kampuni ya Acacia ni kuona Tanzania inapata wataalamu wengi katika fani za Sayansi, ambao watasaidia katika maendeleo ya taaluma hii” Alisema Injinia Philbert Rweyemamu.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Josephine Matiro ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa namna ambavyo umekuwa ukishirikiana na wananchi wa Shinyanga katika kukamilisha miradi mbalimbali. “ Wananchi wetu wengi ni wa kipato cha chini, msaada huu mlioutoa ni mkombozi kwao lakini pia kwa watoto wetu maana mmetutengenezea mazingira mazuri ya watoto wetu kusoma na hapana shaka hawa watabadili hali ya maisha yetu na kuwa mazuri pindi watakapohitimu masomo yao” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni naibu Waziri ofisi ya makamu ya rais Mh. Steven Maselle amesema uwepo wa wawekezaji hapa nchini umekuwa ni chachu ya maendeleo, kutokana na ushiriki wao katika kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imekuwa ya manufaa kwa jamii.
Mbali na utekelezwaji wa ujenzi wa maabara hizi za manispaa ya Shinyanga, katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita  Acacia ilikabidhi pia maabara nyingine kwa Shule ya Sekondari Kinaga katika wilaya ya Kahama ambapo mradi huo uligharimu shilingi milioni mia moja na sitini pamoja na nyumba 3 kwa waathirika wa tukio la mvua za Mwakata zenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania milioni mia moja.
Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi Pamoja na migodi  mingine ya Bulyanhulu na North Mara itaendelea kushirikiana na jamii zinazotuzunguka katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa  jamii na hasa katika maeneo ya afya, elimu, barabara, maji, pamoja na utoaji wa elimu  ya ujasiliamali kwa vikundi mbalimbali. Injinia Philbert Rweyemamu.
Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post