AU KUMCHAGUA MWENYEKITI MPYA WA TUME.

Wagombea wa wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya AU
Viongozi wa nchi za Afrika wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa kikao cha kila mwaka cha Muungano wa Afrika AU.
Moja wa masuaLa makuu kwenye ajenda ni kuchagua mwenyekiti mpya wa tume ya AU kufuatia kukamilika kwa muhula wa mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini-Zuma kutoka Afrika Kusini.
Wagombea watano wanaowania wadhifa huo ni pamoja na waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswanda Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea Mba Mokuy.
Wagombea na wafuasi wao wamekuwa wakifanya kampeni kote barani Afrika kutafuta uungwaji mkono wa nchi wanachama.
Bi Dlamini Zuma ndiye mwenyekiti anayeondoka
Serikali ya Kenya kwa mfano ilifanya kampeni kubwa ya kutafuta kura kwa Bi Mohamed.
Kitamaduni wadhifa huo umekuwa ukizunguka kati ya nchi zanazozungumza lugha ya kiingereza na zile zinazozungumza lugha ya kifaransa.
Bi Dlamini Zuma kutoka nchini inayozungumza lugha ya kiingerea ya Afrika Kusini alichukua wadhifa huo kutoka kwa Jean Ping mwaka 2012 ambaye anatoka nchini Gabon.
Wagombea kutoka mataifa yanayozungumza lugha ya kifaransa ya Chad na Senegal yanaweza kuwa katika nafasi nzuri ikiwa tamaduni hii itafutwa.
Chanzo;BBC Swahil

Post a Comment

Previous Post Next Post