DC WA TANGANYIKA, SALEHE MHANDO AKAGUA SHUGHULI MBALI MBALI ZA UVUVI ZIWA TANGANYIKA MKOANI KATAVI

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Mhe, Salehe Mhando amefanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli mbali mbali za uvuvi wa samaki aina ya Sangara na Dagaa katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika.

DC Mhando amesema ziara hiyo inalenga kuangalia fursa mbalimbali zilizopo na kuwawezesha wavuvi hao wadogo wadogo. Pichani DC Mhando wa pili kulia akipata maelezo akipata maelezo kuhusiana na mradi huo wa kukausha dagaa.
Samaki aina ya Saranga kama aonekanavyo marabaada ya kuvuliwa katika ziwa Tanganyika.
Mmoja wa akina mama wajishughulishao na mradi wa ukaushaji wa Dagaa pembezoni mwa Ziwa Tanganyika, akimuelezea DC Mhandochangamoto mbalimbali wazipatazo kwa suala zima lasoko pamoja na usafiri.

Post a Comment

Previous Post Next Post