Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangalla akiwa na baadhi ya watumishi wa hospitali ya rufaa ya Kitete mkoani Tabora, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo.
………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku siku 7 kwa Katibu Mkuu kumaliza changamoto zinazoikumba hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo mkoani Tabora.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Kitete Mkoani Tabora na kukagua miradi ya chumba cha upasuaji pamoja na Chuo cha AMOS kilichopo mkoani humo .
“Chumba hiki cha upasuaji na Chuo vimekamilika mpaka thamani za ndani tangu miaka miwili iliyopita Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa counter-part funding huku Benki ya Maendeleo ya Afrika ikiwa imetimiza ahadi yake kwa asilimia mia moja”alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa amefurahishwa kutekelezwa kwa baadhi ya maagizo aliyoyatoa kama vile kuondoa msongamano wa wagonjwa kwenye wodi za wanawake wajawazito na watoto.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo umefanikiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa zote muhimu na huduma kwa wateja ikiwemo lugha nzuri kutoka kwa wahudumu imeboreshwa..
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema anashukuru uongozi wa Hospitali hiyo kwa kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya wodi za wagonjwa na sasa hakuna tena msongamano na huduma zinatoka kwa wakati sahihi.
Post a Comment