Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya
ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90,
kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.
Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema
aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa
mafuta yaliofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.
Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati
ya sumu kali kabisa.
Maafisa wa polisi wa Malaysia wanasema wataanza kufagia uwanja huo
wa ndege ambapo shambulio hilo lilifanyika siku 12 zilizopita ili kuchunguza
sumu yoyote iliosalia.
Maafisa wa polisi wa Malaysia walivamia nyumba yake huko Kuala
Lumpur mapema wiki hii ili kuchunguza mauaji hayo.
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo ,huku washukiwa
wengine saba waisakwa na polisi ikiwemo raia wanne na Korea Kaskazini.
Chanzo BBC Swahil.
Post a Comment