- WATU KUMI NA MOJA (11) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA WAKISAFIRISHA MAZAO YA MISITU MBAO ZINAZOKADIRIWA KUWA KIASI CHA ELFU TATU (3,000) WAKIWA KWENYE BOTI TATU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI SENGEREMA.
- MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI NA PIKIPIKI WILAYANI MAGU.
KATIKA TUKIO LA KWANZA;
KWAMBA TAREHE 23.02.2017 MAJIRA YA SAA 16:00 KATIKA KISIWA CHA KOME MCHANGANI KILICHOPO KWENYE ZIWA VICTORIA WILAYA YA SENGEREMA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU KUMI NA MOJA WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1.PHILIPO PETER MIAKA 28, MSUKUMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MGANZA, 2.MAJALIWA ABDALLAH MIAKA 32, MKAZI WA MGANZA, 3.THOBIAS EMMANUEL MIAKA 33, MZINZA MKAZI WA KIJIJI CHA MGANZA, 4.MANENO PETER MIAKA 18, MSUKUMA MKAZI WA KIJIJI CHA MGANZA, 5.SHEDRACK FAUSTINE MIAKA 24, MJITA MKAZI WA BUKOBA, 6. KITUKULA MUNYEMBE MIAKA 39, MJITA MKAZI WA MUSOMA.
WENGINE NI 7, DOTTO ROMA MIAKA 45, MZINZA MKAZI WA MAISOME, 8.JOHN EMMANUEL MIAKA 36, MUHA MKAZI WA KIJIJI CHA MGANZA, 9.RICHARD MWITA MIAKA 27, MKURYA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MGANZA, 10.JONES JONATHAN MIAKA 19, MHAYA NA MKAZI WA MGANZA NA 11.MWESI HANGERE MIAKA 30, MHAYA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MGANZA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA WAKISFIRISHA KIMAGENDO MAZAO YA MISITU MBAO ZINAZOKADIRIWA KUWA KIASI CHA ELFU TATU (3,000) NA MKAA KWENYE BOTI TATTU ZINAZOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.MV SAFARI NNE, 2.MV SAFARI TANO, ZOTE MALI YA SOPHIA ZACHARIA MKAZI WA CHATO NA 3.MV KILIMANJARO MALI YA GEORGE KIMARO, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KUNAMZIGO MKUBWA WA MAZAO YA MISITU MBAO PAMOJA NA MKAA AMBAO UNASAFIRISHWA KIMAGENDO ZIWANI., POLISI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA JUU YA TAARIFA HIZO KWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAMU WA IDARA YA MISITU AMBAPO ASKARI WALITUMIA BOTI ZA POLISI AMBAZO ZINAKASI KUBWA NA KUFANYA MSAKO MKALI ZIWANI VICTORIA NA KUFANIKIWA KUKAMATA BOTI TATU TAJWA HAPO JUU ZIKIWA NA MZIGO WA MBAO NA MKAA PAMOJA NA WATUHUMIWA KUMI NA MOJA KATIKA KISIWA CHA KOME MCHANGANI KILICHOPO WILAYA YA SENGEREMA
AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA KUWA MZIGO HUO WA MBAO ULIKUWA UNATOKEA MKOA WA KIGOMA KUPITIA GEITA NA KUPITISHWA KIMAGENDO ZIWANI ILI KUKWEPA KODI. POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI KUHUSIANA TUKIO HILO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILI WATUHUMIWA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA DHIDI YAO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKAO WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI DHIDI YA WAHALIFU WA AINA YEYOTE ILE ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, AIDHA ANAWATAKA WAFANYA BIASHARA WA MAZAO YA MISITU KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISITU KAMA ZINAVYO ELEKEZA ILI KULIPA KODI YA SERIKALI.
KATIKA TUKIO LA PILI,
MNAMO TAREHE 24.02.2017 MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU KATIKA BARABARA YA MWANZA – MUSOMA KIJIJI CHA KISAMBA WILAYA YA MAGU JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.282 DEE AINA YA TOYOTA LAND CRUISER VX, LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE KELVIN MATAGO MIAKA 26,MKAZI WA TARIME LIKITOEA MWANZA KUELEKEA TARIME LIKIWA KWENYE KASI LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA T.740 BLD AINA YA BOXER AITWAE MOSES THEONES MIAKA 27, MHAYA, CLINICAL OFFICER HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU NA MKAZI WA NYANGUGE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
INADAIWA KUWA GARI TWAJWA HAPO JUU LILILOKUWA LIKITOKEA MWANZA KWENDA MUSOMA LILIKUWA LIMEMBEBA MBUNGE WA VITI MAALUMU CHADEMA ESTER MATIKU, AMBAPO INADAIWA KUWA DEREVA WA GARI ALIKUWA KWENYE KASI AMBAPO ALISHINDWA KULIMUDU GARI KISHA KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI AMBAYE NI CLINIC OFFICER NA KUPELEKEA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
DEREVA WA GARI AMEKAMATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA NDUGU, JAMAA, NA JAMII YA WATU WA WILAYA YA MAGU KWA KUONDOKEA NA MTAALAMU WA AFYA KATIKA AJALI HIYO, JESHI LA POLISI LITAHAKIKISHA SHERIA INAFUATWA NA HAKI INATENDEKA. AIDHA ANAENDELEA KUWASIHI WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABANI ILI KUEPUSHA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WAPOLISI (M) MWANZA
Post a Comment