BABA AMLAWITI MWANAE WA MWAKA MMOJA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari wa Iringa juu ya matukio mbalimbali yaliyojitokeza mkoa humo.

……………………..

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Amani Martin  mkazi wa kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na  kumsababishia maunivu makali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema  mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumshika mtoto kwa nguvu  na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto kuondoka kwenda kuokota kuni na kumuacha mtoto akiwa na baba yake.

Kamanda Bukumbi amesema kiini cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.


Post a Comment

Previous Post Next Post