Duniani kote zaidi ya wanawake na wasichana milioni 200 walio hai leo wamepitia ukeketaji.

  UNFPA Sudan Wasichana wana kamati ya klabu ya shule wakishiriki katika kikao cha kuhamasisha jamii kuhusu   kwa nini ukeketaji wa wanawake una madhara.

Jumuiya ya Zahraa, iliyoko nchini Sudan imeunga mkono harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu duniani, UNFPA kuhakikisha ukeketaji wa wanawake na wasichana, FGM, umetokomezwa. Hii inatokana na kwamba wazazi katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum wanaelimishwa na wanachama wa mtandao wa ulinzi wa jamii kuhusu madhara ya FGM.

Mimi binafsi nilipitia ukeketaji na madhara yake. Sitaruhusu binti zangu kupitia hali hii,” alisema Zuha kutoka jimbo la White Nile, kusini mwa Sudan kupitia makala ya UNFPA.

Baada ya kuhamia Khartoum, Zaha alishtuka kujua kwamba mabinti wa wengi wa majirani zake hawakuwa wamekeketewa, "Sikujua kuwa inawezekana kutomkata binti yangu."

Zuha aliolewa mwaka wa 2009 na kuhama na mume wake mpya, Hashem, hadi Khartoum. Ukeketaji umekuwa ukifanywa sana katika kijiji chake, lakini baada ya kujifungua binti yake wa kwanza, wanachama wa mtandao wa ulinzi wa jamii huko Khartoum walikuja kumtembelea.

Takriban asilimia 90 ya wanawake na wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49 nchini Sudan wamekeketwa kwa namna fulani. Ingawa kiwango kimepungua kutokana na kuharamishwa kwake mwaka 2020 na kuenea kwa juhudi za uchechemuzi na habari, watoto wengi wachanga bado wako katika hatari ya kufanyiwa kitendo hiki cha unyanyasaji wa kijinsia na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kutokomeza mila potofu kuanzia shuleni

Zahraa, msichana mwenye umri wa miaka 12 na mwanafunzi eneo la Town Three  huko Wad Al-Mahi katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan anasema, “ nitaendelea na masomo, sitaolewa hadi nimalizie masomo yangu. Sitaruhusu binti zangu wakeketwe .”

UNFPA inafanya kazi na mtandao wa vijana wa Y-Peer kuanzisha vilabu vya wasichana katika shule za mitaa ambapo vijana wanaweza kuzungumza kuhusu mila hiyo na kujifunza jinsi inavyoweza kuwa na madhara kwa wasichana na wanawake.

Hapo awali, mpango huo ulikabiliwa na upinzani kutoka kwa wazazi ambao hawakutaka watoto wao kuzungumza dhidi ya ukeketaji, lakini kwa kuwashirikisha walimu na viongozi wa kidini katika juhudi za utetezi, wazazi hatimaye walifikia wazo hilo.

Takriban wanafunzi 20 walichaguliwa na kufundishwa kuongoza shughuli za klabu, ikijumuisha mijadala ya vikundi na ukumbi wa michezo shirikishi.

Jumuiya ya Zahraa sasa inaunga mkono hadharani juhudi za kuacha ukeketaji na imejitangaza kuwa haina mila hiyo. Vilabu vya shule vilipata umaarufu mkubwa hivi kwamba watu wanaoishi katika eneo hilo na zaidi katika mkoa huo, wengi wao wakiwa wanawake, waliomba programu zingine zinazofanana na hizo ziandaliwe, na kutoa wito kwa mipango kazi inayoongozwa na vijana, uhamasishaji juu ya usawa wa kijinsia na kutoa wito bora. tahadhari za afya na usalama kwa vijana.

Hali ni tete duniani, UNFPA yataka hatua zaidi

Duniani kote zaidi ya wanawake na wasichana milioni 200 walio hai leo wamepitia ukeketaji. Na mwaka huu wa 2023, takribani wasichana milioni 4.3 wako hatarini kukumbwa na FGM huku UNFPA ikikadiria kuwa kutokana na COVID-19 kuvuruga mipango ya uchechemuzi, wasichana wengine milioni 2 wako hatarini katika muongo ujao kutumbukizwa katika FGM iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa.

Chanzo: Umoja wa Mataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post